29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mameneja wa Tanesco watakiwa kuunganisha wateja

Zuena Msuya- Tabora

NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema mameneja wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) waongeze idadi ya wateja kwa kuwaunganishia huduma ya umeme wananchi waliopo vijijini kwa bei ya Sh 27,000.

Hatua hiyo ni kigezo cha kupima utendaji kazi wa mameneja hayo katika kanda, mikoa pamoja na wilaya mbalimbali nchini.

Mgalu alisema hayo kwa nyakati tofauti, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa Umeme Vijijini,( REA) katika Wilaya za Ulyankhulu, Kaliua, Urambo pamoja na Sikonge Mkoani Tabora,  ambapo aliwasha umeme katika makazi ya watu, nyumba za ibada,taasisi za umma, visima vya maji pamoja na kuzungumza na wananchi wa eneo hayo.

Akiwa katika wilaya hizo, Mgalu aliwasha umeme katika kijiji cha Limbula na Kasunga wilayani ni Kaliua, vilevile katika Kijiji cha Mfindo  wilayani Ulyankhulu.

Aidha akiwa katika wilaya Urambo aliwasha umeme katika kijiji cha Wema, pia aliwsha umeme katika kijiji Kikungu wilayani Sikonge  na kuzungumza na wananchi.

Alisema mameneja wa maeneo husika ndiyo wenye dhamana kubwa ya kuwafuata wateja katika makazi na kuwashawishi kuunganishwa na Umeme badala ya kukaa Ofisini na kusubiri wateja.

“Mradi wa REA umekwisha viunganisha na kuwasha umeme katika vijiji vingi vya wilaya mbalimbali,  naawaagiza mameneja kufanya kazi ya kuwafuata wananchi huko walipo mkawape elimu ili muwaunganishe na umeme, kwa bei ya shilingi 27,000, tunataka kuona idadi ya watumiaji Umeme inaongezeka,” alisema Mgalu.

Tangu mradi wa REA umeanza tayari zaidi ya wateja laki tisa(900,000) wameungamishwa na umeme na bado zoezi hilo linaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles