Elba akanusha kuachana na mke wake

0
572

ElbaLONDON, ENGLAND

MKALI wa muziki na filamu nchini Uingereza, Idris Elba, amekanusha uvumi wa kuachana na mke wake, Naiyana Garth ambao ulianza kuvuma tangu Februari mwaka huu.

Nyota huyo amekanusha habari hizo mara baada ya kuwasili katika tamasha la British Academy Television Awards (Bafta TV), akiwa na mke huyo huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa wawili hao wakiwa pamoja.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo aliweka wazi kwamba bado yupo pamoja na mkewe huyo.

“Ujio wangu katika tamasha nikiwa na mke wangu ni wazi kwamba bado tupo pamoja, ninaamini kuna mambo yameandikwa sana kwenye mitandao ya kijamii ambayo hayana ukweli na ukweli utabaki kwamba bado tupo pamoja,” aliandika Elba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here