22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Dully Sykes kumtoa upya Tanzanite

dullyNA GLORY MLAY

MKALI wa wimbo uliozua zogo wa ‘Uchawi na wanga’ uliodaiwa kujibu wimbo wa ‘Mbagala’ wa msanii Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Athumani Mwingereza ‘Tanzanite’ kwa sasa amedondokea katika studio za msanii mwenzake, Dully Sykes.

Baada ya wimbo huo kuzua utata, nyimbo nyingine za msanii huyo, ‘Radhi’ aliomshirikisha Kitale na ‘Umeniaga’ aliomshirikisha Nay wa Mitego hazikushika chati kubwa kama ilivyokuwa wimbo wa ‘Wachawi na Wanga’.

“Nilikuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu nipo kwenye maandalizi mazito ya nyimbo zangu mbili mpya ambazo nataraji kuzirekodi katika studio za Dully Sykes na More fire.

“Unajua ukimya wangu unatokana na kuhangaika kwa muda na kukosa msimamizi wa kazi zangu ambapo licha ya kujaribu kuomba msaada kwa wasanii wenye majina makubwa sikupata msaada wowote hadi Dully aliponikubalia kunirekodia nyimbo hizo mbili,’’ alieleza kwa masikitiko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles