23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm akiri kuzidiwa kimchezo

KOCHANa Pendo Fundisha, Mbeya

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans van Pluijm amesema kuwa matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya yalitokana na timu yake kuzidiwa  kimchezo.

Matokeo hayo kwa Yanga yameifanya kufikisha pointi 40 na kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza michezo 17, licha ya sare na kufungwa  mabao 2-0  dhidi ya Coastal Union.

Akizungumza juzi baada ya mchezo huo dhidi ya Prisons, Pluijim alisema kuwa wachezaji wake walicheza kwa umakini mkubwa licha ya dakika za mwanzo timu kuonekana kuzidiwa.

Pluijm alisisitiza kuwa wachezaji wake walionekana kuzidiwa na kubadilika kadiri mchezo ulivyoendelea, jambo ambalo lilisaidia kuiweka timu hiyo katika wakati mzuri na kufanikisha kupata  bao  la kwanza dakika ya 35 kipindi cha kwanza.

“Tulipoteza nafasi nyingi lakini ndio mchezo ulivyo, tunajipanga kwa michezo inayofuata hata hivyo wachezaji wangu wamecheza na kujituma sana uwanjani,” alisema.

Naye kiungo wa timu hiyo, Haruna Niyozima, aliwaomba mashabiki wa timu hiyo wasikate tamaa   na kuongeza kuwa mpira siku zote ni matokeo.

“Mpira ni matokeo na haya ni matokeo licha ya mimi na wenzangu kujituma uwanjani katika kutafuta ushindi mwisho wa siku tumepata  sare, ninachowaomba mashabiki wasikate tamaa timu imejipanga katika kuchukua ubingwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles