22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Tulia kuburuzwa mahakamani

tuliaNa Arodia Peter, Dodoma

MBUNGE wa Simanjiro, James ole Millya (Chadema), amesema endapo hatatendewa haki kwenye shauri aliloliwasilisha kwa Spika kuhusu nia ya kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, atakwenda mahakamani.

Alisema ameanza kupata wasiwasi wa namna shauri hilo linavyoendeshwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ambayo alidai   imepelekewa shauri hilo na Dk. Tulia ambaye ndiye mdaiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dodoma jana, Millya alihoji uhalali wa kamati hiyo kushughulikia shauri hilo ilhali mwenye mamlaka ya kulisikiliza ni  Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye yuko   India kwa matibabu.

Mbunge huyo alisema ameshangazwa kesi hiyo aliyoipeleka kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inafanywa kwa usiri na upendeleo wa wazi  ambako wajumbe wa kamati hiyo wanaotokana na Ukawa wameondolewa kinyemela bila hoja za msingi.

“Juni Mosi mwaka huu nilipeleka mashtaka dhidi ya Naibu Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 138, kwa kuwa ndugu Ndugai hakuwapo,  Katibu wa Bunge alipokea kama utaratibu ulivyo. Hadi sasa spika hajarudi ofisini,” alisema.

Akielezea kile alichokiita kupigwa danadana na Kamati hiyo, Millya alisema aliitwa kuhudhuria kikao na kamati hiyo  Juni 18 saa 4.00 kamili mwaka huu, lakini hakuitwa kuingia kwenye kikao hicho hadi saa 9.00 alasiri na baadaye alipewa taarifa kuwa kikao hicho kiliahirishwa hadi Juni 23, mwaka huu.

“Hata hivyo leo (jana) Juni 23 mwaka huu Katibu wa Kamati hajanipa taarifa ya kufika mbele ya Kamati hadi saa 5:15 asubuhi.

“Nilimtumia ujumbe wa simu kujua ni muda gani ninatakiwa kuhudhuria kikao hicho, cha ajabu katibu alikaa kimya na baadaye aliniambia ni saa 5:00. Nilimjibu mbona muda huo umeshapita, alijibu kwamba akidi imetimia na kikao kimeshaanza,” alisema.
Akitoa ufafanuzi wa madai hayo, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, alisema si kweli kwamba Kamati ya Mkuchika inashughulikia suala hilo kwa maagizo ya Naibu
Spika Dk. Tulia, bali ni agizo la Spika, Ndugai ambaye aliwaagiza waendelee na shauri hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles