28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mselly: Serikali ifikirie upya mikakati yake ilete tija

Dk. Mselly Mbwambo Nzota.
Dk. Mselly Mbwambo Nzota.

NA SARAH MOSSI,

WIKI iliyopita tulichapisha sehemu ya kwanza ya mahojiano kati ya Mwandishi SARAH MOSSI aliyefanya ziara ya kikazi nchini Sweden hivi karibuni na Mtanzania Dk. Mselly Mbwambo Nzota ambaye ni mtaalamu katika mambo ya utengenezaji  chuma katika eneo la Research Development.

Dk. Mselly ni miongoni mwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi wenye uchu wa kusaidia Watanzania wenzao katika nyanja mbalimbali lakini wameliwa wakikwamishwa na sababau ambazo haziko wazi.

Katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na Dk. Mselly anaeleza ndoto yake kubwa ni kuwekeza katika elimu na kwa maneno yake alisema aliona kuwekeza upande wa elimu ndio kitu cha maana kuliko kwenda kujenga vitu vya ajabu. Endelea na sehemu ya pili ya makala haya….

MTANZANIA: Kwa maoni yako unafikiri ni kwanini nchi yetu inakwama katika baadhi ya mambo?

Dk. MSELLY: Kuna vitu viwili ambavyo vinafanya nchi yetu isiendelee, cha kwanza sisi Watanzania tulikuwa hatujui kama tunaibiwa, katika misitu tulikuwa hatujui kama pale kuna mali inakwenda na katika madini, sasa ukishaanza kufukua na wananchi wakagundua kama walikalia utajiri, utakwamishwa.

Kwahiyo utaona namna nilivyojitolea na mimi naamini elimu yangu ndio muhimu zaidi katika kuwanyanyua Watanzania wenzangu.

MTANZANIA: Moja ya vilio vya Diaspora ni kukwamishwa pale wanaporudi nyumbani kutaka kuwekeza au wanachukuliwa ni kama vile wageni kabisa kaika nchi yao mama, hili wewe unalionaje?

MSELLY: Tufanye kama Rwanda, alichofanya Kagame kwamba Mrwanda yeye anayeishi nje akitaka kurudi arudi ajenge nchi na mawazo yao yanakaribishwa, Ndio maana ile nchi katika muda mfupi tu ikabadilika, lskini sisi tulioko nje tunachezewa tu. Mimi niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Mazingira kaika Sweden yote na ukiona Mswidi amekupa kazi hiyo ujue amekuamini.. Waswidi wananiamini lakini Watanzania hawaaki kuniamini. Mimi kila baada ya miezi miwili pale kazini kwangu napelekwa nje ya  nchi kuzungumzia.

MTANZANIA: Unaionaje hii kauli ya Rais kwamba anataka Tanzania iwe ya uchumi wa Viwanda?

MSELLY: Kama alivyosema Rais, Kama kweli tunataka kuwa nchi ya viwanda lazima tuwe serious katika hili kwanza kile kiWanda cha chuma tujue kwamba kinataka kufanya nini, tunaamua kutengeneza Construction steel au kiwanda cha kutengenezea masufuria, ni lazima Serikali ijue hilo, au tunataka tuuze kama raw materials ambayo Wachina ndio wanaifuata ka sababu wameshajua sisi hatujui na kama mtu hujui wanakudanganya wanachukua, sio wajinga wale.

Mimi nafikiria kwamba jambo la muhimu ni kwamba Serikali iwe serious na hakuna mtu mwingine ambaye anaweza akafanya hiyo kazi kama sio Serikali. Serikali tu iipe kipaumbele kama proudly of a country wajue kama chuma ndio kinaendesha jeshi na ndio kitu cha maana. Na sio kama nasema kwa ajili ya utaalamu wangu.

MTANZANIA: Kwa kipindi cha miaka fulani tatizo lilikumbwa na kashfa ya baadhi ya watu kuuza vifaa vya ujenzi vya visivyo na ubora hususani nondo na kusababisha baadhi ya majengo kuanguka, unafikiri tulikosea wapi kama Taifa?

MSELLY: Ndio kile nilichosema kwamba kama taifa kuwe na maabara na Shirika la Viwango (TBS), liwe na wataalmu wa kuangalia kwamba kitu hakiendi, pengine haina wataalamu wazuri na kama wapo basi wanapewa hiyo dili.

Mimi nilifika pale, ukishavunja nondo kwa mkono ujue hicho ni kitu kichafu, huwezi kuamini, nondo inavunjika, liliposhuka jengo pale katikati ya Jiji la Dar es Salaam, mimi nilifika kwa yule muhindi na hata kule VETA Arusha nilipofika niliona hawana maabara.

Kwa mfano ule mchanga wote pale bandarini ile ni malighafi unaweza kutengeneza glasi, lakini hakuna maabara ya kupima

Kwa hiyo mimi mawazo yangu ndio hayo ni kwamba I think ni lazima tu re-think about our strategy, tusiseme tu ili kupata kura, ni lazima tuangalie strategu zetu, Je, zinakwendaje? Kwa mfano tuangalie watu muhimu kwa mfano hata mimi usiponilipa, tiketi ni kitu kidogo sana, kama Serikali inaniambia Dk. Mselly kuna kitu cha haraka sana tunasaka utupe mawazo haya.

Usiwe unatoa uamuzi wa vitu ambavyo uwezo huna, Unakaa na Wachina unadiscuss na kuhusu chuma chuma wakati hata siku moja hujafanya utafiti wa chuma kujua whaa is it, Ni muhimu kuwatumia Diaspora wenye utaalamu, ndio maana nilisema ile Dara Base iliyoanzishwa ni muhimu sana, ni lazima itumike sio imeanzishwa tu na itumike kwamba kama kuna utaalamu unatakiwa basi tuwajue wapi walipo wataalamu wetu duniani kote. Ofisi za ubalozi zitumike kuwatambua waaalamu hao  na kuwaomba watalaamu ajitokeza, tuwe wazi katika hili.

Lakini kama hatuendi hivyo its over, sasa kwanini walinituma mimi nikasome Bulgaria, walinituma nikacheze? Rais wetu kama anao uwezo inatakiwa nchi iweke priority. Kama si hivyo hatutofika mbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles