27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

DK. MPANGO ASOMA ‘SMS’ YA MKOPO BUNGENI

Gabriel Mushi, Dodoma

Hatimaye Serikali ya India imekubali kutoa mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 (trilioni 1.1) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya maji nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ambaye alisoma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), aliotumiwa leo kuhusu kumalizika kwa utata wa fedha hizo.

Amesema Aprili 15, mwaka huu serikali iliridhia kusamehe kodi zote za mapato ambazo Serikali ya India iliweka masharti ya kutaka kusamehewa.

“Niliarifu bunge lako tukufu kuwa saa 11: 27 nimeletewa taarifa naomba nisome, kindly be formed that we have successfully concluded the negotiations with Exim bank of India, we will sign the agreement tomorrow morning. Inshallah!

“Hii ni taarifa ambayo nimeletewa na kiongozi wa timu ya wasuluhushi wa suala hili katika serikali ya India kwa jili ya kumaliza zoezi hili,” amesema.

Dk. Mpango amesema fedha hizo zilichelewa kupatikana kwa sababu serikali ya India iliendelea kusisitiza kuwa lazima zisamehewe kodi zote, tozo na VAT.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles