22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Jingu: Wakulima tuongeze msukumo wa kufanya kilimo chenye tija

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dk. John Jingu ametoa rai kwa wakulima kuongeza msukumo katika kilimo chenye tija kwa kutumia mbinu za kisasa za kilimo ambazo zinahusisha teknolojia ili kuleta matokeo mazuri zaidi.

Makatibu Wakuu na Wadau wa Kilimo wakiwa katika Kikao cha Tathimini ya Usimamizi na Ushauri wa Programu ya Kuendeleza Kilimo Awamu ya Pili kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam.

Wito huo ameutoa katika kikao cha Kamati ya Tathmini ya Usimamizi na Ushauri wa Programu ya kuendeleza Kilimo Awamu ya Pili kilichohusisha Makatibu Wakuu na Wadau wa Kilimo kilichofanyika Februari 17, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Saalam.

Dk. Jingu amesema dhamira ya Serikali ni kuona wakulima wanatumia rasilimali kidogo na kupata faida zaidi.

Aliongezea kuwa serikali itaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kufanya katika kuimarisha sekta ya kilimo na mifugo ili kuongeza ufanisi kwa manufaa ya Taifa.

“Mwelekeo ni kwamba shughuli wanazofanya ziwe na mwelekeo wa kibishara kwa maana kilimo ni biashara na uvuvi ni biashara,” amesema Dk. Jingu.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Nazael Madalla amesema uvuvi nchini bado unatumia mbinu za zamani nakwamba kwa sasa wanaenda kutoa boti mpya za kisasa zitakazofanya wavuvi waongeze tija.

Ameongeza kwa kusema kuwa, jitihada hizo zinaenda sambamba na kutoa mikopo kwa wafugaji wa samaki kwenye vizimba katika ziwa Viktoria kwa kuwapatia vizimba vya samaki na vifaranga vya samaki na chakula cha samaki.

“Lengo ni kuongeza uzalishaji wa samaki na kutimiza malengo tuliyopewa na Mhe. Rais wa kuongeza tani za uzalishaji wa samaki ifikapo Mwaka 2026,” amesema Dk. Madalla.

Aidha, amesema serikali imeahidi kuendelea kutoa mikopo kwa wakulima wa mwani katika ukanda wa Pwani ili waweze kununua vifaa na kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Maduhu Kazi amesema Mpango wa Usimamizi na Ushauri wa Program ya Kuendeleza Kilimo Awamu ya Pili ni jumuishi unaohusisha wizara kupitia Jeshi la Magereza na Jeshi la Polisi  ambayo yanajihusisha na shughuli mbalimbali za kilimo na uwekezaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles