31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kliniki ya Huduma Rafiki kwa Vijana yazinduliwa Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Shirika la Umoja wa Mataifa Linalo Shughulikia Maswala ya Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi mashine mbili za ultrasound zinazohamishika kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar, zitakazosaidia huduma za kuwafikia kina mama wajawazito ili kubaini matatizo na kusaidia mimba salama.

Hafla hiyo imefanyika Februari 15, 2023 katika Kliniki ya Huduma Rafiki kwa Vijana ilizinduliwa Bumbwisudi, Zanzibar Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Zahanati ya Huduma Rafiki kwa Vijana ilikarabatiwa chini ya Mradi wa Wezesha Wasichana, ambao unatekelezwa kwa pamoja na UNFPA na UNICEF, na kufadhiliwa na Serikali ya Canada.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Mazrui amesema kuwa msaad huo utawasaidia vijana kupata ushauri pindi wanapotumia njia za uzazi wa mpango.

“Vijana wengi wamekuwa wakitumia njia za uzazi wa mpango bila kufuata ushauri wa wataalam wa afya jambo ambalo linawasababishia madhara kiafya na kudhani kuwa njia hizo si salama, lakini tatizo ni taarifa zisizo sahihi.

“Bila shaka, Kliniki hii ya Kituo cha Huduma za Kirafiki kwa Vijana itawawezesha vijana kupata taarifa kwa wakati na huduma za kitaalamu,” amesema Mazrui.

Akizungumza wakati wa hafala hiyo Mwakilishi Mkazi Mkaazi wa UNFPA, Mark Bryan Schreiner amesema kuwa vijana wanahitaji kupata huduma na taarifa ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi.

“Idadi ya vijana wenye nguvu nchini Tanzania inaongezeka. Vijana wanahitaji kupata huduma na taarifa ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi, ikiwa ni pamoja na kuhusu afya yao ya ngono na uzazi.

“Huduma Rafiki kwa Vijana zinasaidia vijana katika kufanya maamuzi yenye afya, na kuhakikisha haki na chaguo kwa wote,” amesema Schreiner.

Akizungumzia mradi wa Wezesha Wasichana ni wa miaka mitano, unaolenga kuboresha afya ya ujinsia na uzazi, haki na ustawi miongoni mwa wasichana walio katika mazingira magumu katika wilaya zote 22 za mikoa ya Mbeya na Songwe na Zanzibar; 2023 ni mwaka wa mwisho wa mradi.

Chini ya mradi wa Wezesha Wasichana, UNFPA imefanya kazi na Wizara ya Afya katika ukarabati wa kliniki tano za Huduma Rafiki kwa Vijana; ya mwisho inaendelea Pemba.

UNFPA pia imesaidia kujenga uwezo wa zaidi ya wafanyakazi 500 katika afya ya ngono na uzazi, na kusaidia uundaji wa miongozo, mwongozo wa mafunzo na usimamizi wa data.

Wizara ya Afya itatenga watumishi wa Huduma Rafiki kwa Vijana wa kusimamia zahanati hizo, ili kuwapatia vijana taarifa na huduma zinazoendana na umri.

Kliniki ya Huduma Rafiki kwa Vijana iliyopo Bumbwisudi ni miongoni mwa zahanati kumi ambazo zimesaidiwa hivi karibuni na UNFPA katika jitihada za kuhakikisha vijana wengi zaidi wanapata huduma za afya ya uzazi na uzazi.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Idris Kitwana Mustapha, Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mjini Magharibi; Hamida Musa, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A; viongozi wa Serikali, wakiwemo maafisa kutoka Wizara ya Afya ya Zanzibar, na wawakilishi kutoka NGOs, asasi za kiraia na kutoka vyombo vya habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles