29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bashiru aipongeza Ofisi ya Mkemia Mkuu

Na Aveline Kitomary, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Dk. Bashiru Ally, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) kwa kupanga mipango ya utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia vipaumbele vya ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba, Hadija Mwema (kulia) akimuonesha Katibu Mkuu Wa Chama Cha Mapinduzi, D. Bashiru Ally (kushoto) Hatua Za kufanya uchunguzi wa Sampuli za Vinasaba kwa masuala ya Kijamii na Jinai unavyofanyika  baada ya Katibu Mkuu Kutembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Februari 16, 2021.

Dk. Bahsiru amesema hayo jana Februari 16, baada ya kutembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kujionea utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo ya Serikali.

“Nimefurahishwa kukuta mipango yenu inaoanisha majukumu yenu na ahadi zilizopo kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 -2025, hili limenifurahisha sana. Kila jukumu mmelionesha kulingana na ilani na namna mtakavyotekeleza kama vile masuala ya haki jinai, utafiti, mazingira, matibabu ya kibingwa, ubunifu, magonjwa ya mlipuko, teknolojia, uchunguzi wa kimaabara na kupunguza kesi mahakamani mmeonesha nafasi yenu ya utekelezaji.

“Mmenipa faraja katika mipango yenu ya kila siku, mwaka na miaka mitano ijayo. Niliyojifunza nitafikisha kwenye Chama na Serikali ili kusaidia kutatua changamoto zenu. Hongereni sana mnafanya kazi nzuri,” amesema Dk. Bashiru.

Katibu Mkuu pia amepongeza uwekezaji mkubwa wa mitambo na vifaa vya maabara uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na kupongeza uzalendo na uadlifu wa watumishi huku akisisitiza kuendelea kusimamia weledi na kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

“Baada ya kupitia nyaraka na kuzunguka kwenye maabara zenu nimebaini mambo makubwa matatu ambayo ni kwanza, Serikali imewekeza vifaa (mitambo) vya kisasa na uwekezaji huo utumiwe kwa makini ili kutunza vifaa. Pili, kuna timu ya kazi yenye uzalendo na nisisitize kwa uzito wa majukumu yenu suala la uadilifu na uzalendo ni jambo muhimu sana. Tatu, kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya majukumu yenu kisheria,” amesema Dk. Bashiru.

Akiongea kuhusu ziara ya Katibu Mkuu, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko, amemshukuru kwa kutenga muda na kutembelea Mamlaka kwa lengo la kuweza kuona utekelezaji wa majukumu yake kwa Serikali na umma wa watanzania.

“Kwa niaba ya Bodi, Menejimenti na Watumishi wote tunaahidi kuendeleza utekelezaji wa kuzingatia rai ulizotupatia na tunayachukua kwa uzito mkubwa haya masuala uliyotuasa na kusisitiza ya uadilifu, uzalendo, utunzaji wa vifaa, mafunzo kwa wataalam na utoaji elimu kwa umma. Tunachoomba kwako ni kuwa Balozi wetu kwa kile ulichokiona,” amesema Dk. Mafumiko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles