27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yasaini mikataba sita ya Sh bilioni 307.9 kuboresha huduma

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Serikali ya Tanzania imetia saini mikataba sita zenye thamani ya Sh bilioni 307.9 iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ajili ya kuboresha sekta ya nishati, huduma za afya ya mimea, mazingira ya biashara na ushirikiano wa kitaalamu.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mikataba hiyo leo Februari 16, jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, amesema Serikali imesaini mikataba sita inayofadhiliwa na EA kupitia Mpango wa Ushirikiano wa 11 chini ya Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (NDF) ambapo amedai jumla ya gharama za miradi hiyo ni Sh bilioni 307.9.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni wa kuboresha sekta ya nishati wenye thamani ya Sh bilioni 96.7, mradi wa matumizi endelevu ya nishati ya kupikia wenye thamani ya Sh bilioni 82.8, mradi wa kusaidia mnyororo wa thamani katika ufugaji nyuki wenye thamani ya Sh bilioni 27.6.

Katibu Mkuu huyo ameitaja miradi mingine kuwa ni wa kuboresha huduma ya afya ya mimea nchini ili kuongeza usalama wa chakula wenye thamani ya Sh bilioni 27.6, mradi wa kusaidia kuboresha mazingira ya biashara na ukuaji wa ubunifu wenye thamani ya Sh bilioni 63.

Aidha, ameutaja mradi mwingine kuwa ni wa kusaidia kuboresha mazingira ya biashara, ukuaji na ubunifu wenye thamani ya Sh bilioni 63.5.

“Kwa niaba ya serikali napenda kuushukuru sana Umoja wa Ulaya kwa misaada yake hii kwa Tanzania kwani imekuja wakati muafaka ambapo serikali inaweka mazingira wezeshi  ya kukuza viwanda kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wetu,”amesema Katibu Mkuu huyo.

Vilevile, amesema hadi sasa Tanzania imepokea kutoka UE Sh trilioni 6.6 kama msaada na Sh bilioni 748 kama mikopo yenye masharti nafuu  kutoka Benki ya Uwekezaji  ya Ulaya (EIB).

Kwa upande wake, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Manfred Fanti, amesema lengo lao ni kuhakikisha bidhaa za hapa nchini zinapata soko Ulaya huku akisisitiza umuhimu wa bidhaa hizo kuongezwa thamani.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk.Aloyce Nzuki amesema Wizara yake inayofuraha kupata miradi miwili ambayo ni wa matumizi  endelevu ya nishati ya kupikia pamoja na ule wa kusaidia mnyororo wa thamani katika ufugaji nyuki.

“Tunashukuru kwa miradi hii kwani kutakuwa na njia mbadala katika suala la nishati matumizi ya kuni yamekuwa yapo juu.Pia thamani ya ufugaji nyuki itaongezeka kwa kuongezewa thamani,”amesema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, ameseishukuru (EU) kwa miradi hiyo ambapo aliahidi Serikali ya Tanzania kuisimamia vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles