26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mufindi yaweka mkakati ukusanyaji kodi za majengo, mabango

Na Raymond Minja, Mufindi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi mkoani Iringa, Netho Ndilito, amewataka watendaji wa kata na vijiji kwenda kuwatambua na kuwahakiki wafanyabiasha kwenye maeneo yao ili kuweza kuweka mkakati bora wa ukusanyaji wa kodi za mabango na ushuru ili kufikia lengo la halmashauri hiyo.

Ndilito ametoa rai hiyo juzi alipokutana na na watendaji wa kata 27 na watendaji wa vijiji 121 kwa lengo la kupanga na kuweka mikakati bora ya ukusanyaji kodi katika halimashauri hiyo .

Amesema halmashauri hiyo ya wilaya ya Mufindi inavyanzo vingi vya mapato lakini vingine huwa vinapotea kutokana na kutokuwa na mpango bora na mkakati mzuri katika ukusanyaji wa kodi katika vyanzo hivyo.

“Ni wajibu wenu kama watendaji kwenda kuwatambua wafanyabiashara katika maeneo yenu, ili kuweka mikakati bora na mizuri ya ukusanyaji wa kodi za majengo na mabango na ninauhakika mtafanya vizuri kwani halmashauri yangu ya Mufindi inawatendaji wazuri, wazalendo na wachapakazi hivyo mutakwenda kufanya zoezi hili kwa ufanisi mkubwa na weledi wa kazi zenu,” amesema Ndilito.

Amesema kuwa katika halmashauri hiyo kuna wafanyabiashara wa aina tatu, wenye TIN number, wenye leseni za biashara na wale wenye vitambulishi vya ujasiriliamali na endapo kuna mfanyabiashara ambaye anafanya biashara na hayuko kati ya hao walioainishwa basi huyo ni muhujumu uchumi wa nchi yake.

Hata hivyo, Ndilito amewataka wafanyabiashara na Watanzania wote kwa ujumla kujenga utamaduni na uzalendo wa kulipa kodi bila kushurutishwa kwani kodi wanazilipa ndizo zinazurudu kuja kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.

Akitoa ufafanuzi kuhusu nani anatakiwa kutozwa kodi ya jengo Afisa Biashara wa Halmashauri hiyo, Raymond Kalinga, amesema miongozo inaonyesha wazi ni nani anatakiwa kulipa na aina gani ya majengo yakulipia au nani asilipe inabainisha wazi hivyo ni vema miongozo hiyo ifatwe na kutozwa kwa usahihi bila ya kuvuruga amani ya nchii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles