31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mfuko wa jimbo wafufua tumaini jipya la miradi ya Ludewa

Na Mwandishi Wetu, Njombe

Zaidi ya Sh milioni 40 ambazo ni fedha kutoka mfuko wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe, zimetumika awamu ya kwanza kwa ajili ya kununua mifuko 1,200 ya saruji pamoja na bati 968 ili kusaidia ukamilishwaji wa maboma ya miradi ya afya na elimu iliyokwama kwa muda mrefu kwenye vijiji na kata jimboni humo.

Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, Wakili Joseph Kamonga, kabla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa madiwani na watendaji wa kata katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika wilayani humo, amesema msaada huo umetolewa ili kusaidia majengo yaliyoanzishwa na wananchi na kukwama kwa muda mrefu angali wananchi wametokwa na jasho wakati wa kuanzishwa kwa miradi.

“Kuna baadhi ya majengo wananchi wamepaua kabisa lakini kuezeka bado, kwenye vijiji na kata wananchi wametoka jasho mpaka wamekuwa wazito kuendelea kuchangia.

“Tumekusanya takwimu kwa picha na jengo kila lilipo na tunaahidi kushughulikia jambo lolote ambalo lina manufaa kwa wananchi wetu bila kujali ni nani aliyelianzisha,” amesema Kamonga.

Aidha amesema ugawaji wa vifaa hivyo ni pamoja na utekelezwaji wa ahadi mbalimbali ikiwemo za ukamilishwaji wa majengo hayo na kuwataka wanachi na kata ambazo hazijapata kwa awamu hii kuwa wavumilivu kwa kuwa imeangaliwa jengo lenye hatua nzuri.

Miradi mingi inayotarajiwa kunufaika na vifaa hivyo ni pamoja vituo vya afya na zahanati, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Dk. Stanley Mlay, amesema halmashauri ina zahanati 18 na vituo vya afya 14 ambayo vipo katika hatua mbali mbali za ujenzi hivyo wanategemea kuongezeka kwa kasi ya ujenzi kupitia misaada hiyo.

“Lakini nitumie nafasi hii kuwashukuru wananchi ambao kwa kiasi kikubwau wamekuwau wakishiriki katika ujenzi wa vituo vya afya na zahanatiu nah ii inaonyesha ni jinsi gani wanauhitaji Piano nimpongeze sana Mbunge wa Ludewa kwa kuwa ametusaidia sana kuhakikisha wananchi wanapunguziwa mzigo kwenye ujenzi kwa kuwa vifaa hivi vitasogeza hatua za ujenzi,” amesema Dk. Mlay.

Baadhi ya madiwani na watendaji wa kata akiwemo, Vasco Mgimba, wa kata ya Ludende na Wilbad Mwinuka wa kata ya Luana, wamesema kutokana mfuko wa jimbo kwa kuwa utakuwa na msaada mkubwa kukamilisha maboma mbali mbali ya afya na elimu katika katahl zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles