22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Djokovic atwaa taji la BNP Paribas

novak-djokovic-indian-wells-trophy_3435071PARIS, UFARANSA

NYOTA wa mchezo wa tenisi namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic, amefanikiwa kutwaa taji la tano la michuano ya wazi ya BNP Paribas, iliyofanyika nchini Ufaransa.

Bingwa huyo ametwaa taji hilo baada ya kumshinda mpinzani wake, Milos Raonic, kwa seti 6-2 6-0.

“Imezidi kuwa siku ya furaha kubwa kwa upande wangu kwa kutwaa taji hili, ninaamini huu ni mwanzo mzuri kwa ajili ya michuano mingine,” alisema Djokovic.

Kwa upande wa wanawake, Victoria Azarenka, amefanikiwa kutwaa taji hilo baada ya kumshinda mpinzani wake, Serena Williams, ambaye ni nyota namba moja kwa ubora kwa wanawake.

Victoria alifanikiwa kuibuka kidedea kwa kumshinda seti 6-4 6-4. Hata hivyo, Victoria amedai kwamba japokuwa wameshinda, lakini alikuwa na ushindani mkubwa na mpinzani wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles