25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Zidane adai Madrid ipo tayari kwa El Clasico

zidane-zinedine-150526-620MADRID, HISPANIA

MADRID baada ya kushinda juzi mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania dhidi ya Sevilla, kocha wa timu hiyo, Zinadine Zidane, amesema kwamba kikosi chake kipo tayari kupambana na wapinzani wake Barcelona.

Matokeo hayo yameanza kumpa jeuri Zidane, ambapo anaamini kuwa anaweza kushinda dhidi ya Barcelona mchezo ambao utapigwa Aprili 2, mwaka huu.

Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou dhidi ya vinara hao wa Ligi ambao kwa sasa wana jumla ya alama 76, ikifuatiwa na Atletico Madrid, ambao wana alama 67, huku Madrid wakishika nafasi ya tatu kwa alama 66.

“Nimekuwa na furaha kubwa kuiona Madrid ikicheza katika kiwango cha hali ya juu dhidi ya Sevilla, tumebakiwa na wiki moja kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Barcelona.

“Najua kwamba kila mchezo unakuwa tofauti kwa kuwa unakutana na wachezaji tofauti, lakini ninaamini kikosi hiki cha sasa kinaweza kupambana vizuri na Barcelona na kupata matokeo mazuri.

“El Clasico siku zote unakuwa ni mchezo maalumu, tunatakiwa kutumia mifumo tofauti kwa ajili ya kujihakikishia ushindi na tuko tayari,” alisema Zidane.

Kwa upande wa vinara wa La Liga, Barcelona, juzi iliambulia sare ya mabao 2-2 dhidi Villarreal kwenye Uwanja wa El Madrigal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles