Director P kufungua mwaka na Show Me

0
333

Na Mwandishi Wetu

Msanii Director P anatarajia kuachia wimbo mpya Januari 9, mwaka huu unaofahamika kama Show Me aliomshirikisha, Golden Boy.

Director P ambaye pia ni mwongozaji wa Video, amesema wimbo huo uliorekodiwa katika Studio za Lupasa Records zilizopo Toronto, Canada, ni mwendelezo wa kazi zake atakazozitoa mwaka huu zikiwemo Mama na Nionyeshe aliomshirikisha, Fidel Sebastian chini ya Producer wa Tanzania.

“Huu ni mwendelezo wa kuwajali mashabiki zangu wa Afrika, kwani haijalishi niko wapi, Afrika ipo na itakuwa nyumbani kwangu kila wakati, nina kazi nyingi ambazo zinatoka mwaka huu zikiwemo video ambazo nimeziongoza.

“Lakini pia kuna kazi zangu mwenyewe ambazo nimeimba mwenyewe na Januari 9, mwaka huu ambayo ni siku ya kuzaliwa kwangu ndio natarajia kuachia Show Me niliyomshirikisha Golden Boy, hivyo namba mashabiki zangu waendelee kuniunga mkono,” amesema Director P mwenye asili ya Zambia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here