Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam
Baraza la sanaa la Taifa (Basata) ambalo ni msimamizi wa sekta ya burudani limemfungia msanii Gift Stanford ‘Gigy Money’ kujishuhulis ha na shughuli za kijana kwa muda wa miezi sita na faini ya shilingi milioni moja.
Gigy Money mwanzoni mwa mwaka huu akiwa katika tamasha la Tumewasha Tour jijini Dodoma, alipanda jukwaani kutumbwiza na kuvua gauni aina ya dera na kubaki na vazi ambalo linaonyesha maumbile yake na kupelekea kudhalilisha utu wake na kubugudhi wadau wa sanaa nchini.
Adhabu hiyo imetolewa leo Januri 5, ambapo Baraza limejirishisha kuwa alikiuka maadili ya sanaa ambapo amevunja kifungu 4 (L) cha sheria namba 23 ya mwaka 1984 (Re:2002), kanuni 25(6) (9) ya kanuni za Baraza za mwaka GNN43/2018 na utaratibu wa uwendeshaji wa shughuli za sanaa.
Gigy Money amesha fikishwa mara kadhaa katika Baraza la Sanaa la Taifa na kuonywa kwa ukosefu wa maadili ambapo mwaka 2017 nyimbo yake ilifungiwa kwa kosa la kutumia misamiati isiyo na maadili.