28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Diarra ampoteza ndugu yake Ufaransa

lassana-diarra-new-photos-4PARIS, UFARANSA

KIUNGO wa klabu ya Marseille ya nchini Ufaransa, Lassana Diarra, amesema kwamba amempoteza ndugu yake katika shambulizi la kigaidi lililotokea juzi mjini Paris nchini humo.

Katika shambulizi hilo limepoteza maisha ya watu wengi huku zaidi ya watu 40 wakijeruhiwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hadi sasa watu zaidi ya 127 wamepoteza maisha baada ya kutokea mashambulizi katika maeneo mbalimbali kwenye miji sita kwa wakati tofauti nchini humo.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Diarra aliandika kwamba mpwa wake alikuwa katika eneo la shambulizi lilipotokea.

“Habari za jioni watu wote, poleni na matukio ya mashambulizi yaliyotokea juzi katika mji wa Paris na St Denis ni jambo la kusikitisha sana.

“Licha ya kuenea kwa taarifa kuhusu watu walioathirika na mashambulizi hayo, pia mpwa wangu, Asta Diakitie, ni miongoni mwa waliouawa kwenye tukio hilo,” aliandika Diarra.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles