Nyota hao ni pamoja na mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2014, Yacine Brahimi kutoka nchini Algeria, Pierre-Emerick Aubameyang kutoka nchini Gabon, Andre Ayew, kutoka Ghana, Sadio Mane na Yaya Toure wa Ivory Coast.
Mshindi ataamuliwa na mashabiki wa soka Afrika ambao watapewa fursa ya kupiga kura hadi ifikapo tarehe 30 Novemba, huku mshindi akitarajiwa kutangazwa Desemba 11 mwaka huu.
Katika kinyang’anyiro hicho, Aubameyang anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na kile ambacho anakifanya katika klabu yake ya Borussia Dortmund ambaye anaongoza kwa kupachika mabao nchini Ujerumani akiwa na mabao 14 hadi sasa.
Hata hivyo, anaonekana kuwa na upinzani mkubwa na mshambuliaji wa klabu ya Swansea City na timu ya taifa ya Ghana, Ayew ambaye anatoa mchango mkubwa katika klabu yake, japokuwa alishindwa kufua dafu katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.
Lakini bingwa atapatikana mara baada ya kupigiwa kura, hivyo mchezaji yeyote anaweza kuibuka na ushindi huo kutokana na vile alivyozisaidia timu zake.