24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond: Tifah wangu si wangu, mniache!

NasibNA MWALI IBRAHIM

MKALI wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul ‘Diamond’ ameshangazwa na watu anaodai ni wakubwa kwake kutaka kushindana naye wakati yeye ni zaidi yao.

Diamond alisema anashangazwa na wanaohangaika kushindana naye wakati yeye anajulikana zaidi yao, akaunti yake haikosi milioni 10 na pia ana mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii.

“Mi nashangaa wasanii wengi wananizonga kuhusu mtoto wangu wanataka nikapime DNA, wao inawahusu nini kama wa kwangu ama si damu yangu, mimi nawashangaa watu wazima wanataka kushindana na mtoto mdogo ambaye kwanza ni staa zaidi yao, najulikana kila nchi niendayo, akaunti yangu haikosi milioni 10, Instagram nina mashabiki wengi kuliko wao, mimi naona bora wapambane kutangaza muziki wao na kujenga nyumba nzuri za kuishi,’’ alijinadi Diamond kupitia kipindi cha Amplify kinachoongozwa na mtangazaji Milard Ayo.

Hayo yalikuwa majibu ya msanii huyo baada ya kuibuka kwa uzushi katika mitandao ya kijamii na mijadala mbalimbali kwamba wasanii wengi wamekuwa wakidai kuwa Tifah si mtoto wake na wanamtaka akapime vinasaba ‘DNA’, kitu ambacho kinamkera ndiyo maana akawataka wamuache na maisha yake nao wahangaikie muziki wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles