27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Double M Plus kurejea nchini ikiwa mpya

Double M muumini mwinjumaNA MWALI IBRAHIM

UJIO mpya wa bendi ya Double M Plus unatarajiwa kufanyika muda mfupi baada ya bendi hiyo kuwasili nchini ikitokea nchini Msumbiji.

Bendi hiyo itawasili mwishoni mwa wiki hii baada ya ziara ya kimuziki iliyofanya nchini humo na pia kuweka kambi ya mazoezi iliyochukua zaidi ya miezi miwili.

Mkurugenzi  wa bendi hiyo, Muumini Mwinjuma ‘Kocha wa Dunia’, alisema baada ya kumaliza maonyesho yao katika miji mbalimbali nchini humo, bendi hiyo iliweka kambi ya mazoezi ambapo ilisukwa upya ili iwe tishio na shindani kwa bendi nyingine zilizopo nchini.

“Bendi imeiva, tupo kamili kutoa burudani na tunawataka mashabiki wetu wawe tayari kutupokea kwa nyimbo za karne tulizowaandalia sambamba na shoo za kutosha,” alieleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles