27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

DIAMOND: NITAFANYA SURPISE YA NGUVU DAR LIVE

d1NA EDO BRIAN

MKALI wa Bongo Fleva Nasibu Abdul a.k.a Diamond Platnumz amesema mashabiki wake wajiandae kwa surprise ya nguvu atakayofanya katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala – Zakheem jijini Dar es Salaam siku ya Krismas.

Akipiga stori na Swaggaz, Diamond alisema mashabiki wake wanamjua kutokana na makali yake, hivyo wasiwe na shaka kwani atafanya shoo ya aina yake itakayowaondolea stress za mwaka mzima uliopita.

Licha ya kwamba hajawahi kuwaangusha mashabiki wake kwenye shoo tangu apate umaarufu takribani miaka sita iliyopita, lakini safari hii ameahidi kufanya mara mbili zaidi ya anavyofanya akiwa kwenye majukwaa mengine
siku za nyuma.

“Waje tu wengi, sijawahi kuwaza kuwaangusha watu wangu, najua Watanzania wanataka nini na nipo hapa kwa ajili ya kuwafurahisha wao na kuzidi kuipeperusha bendera yaTanzania.

Nitafanya zaidi ya huko nyuma, nataka kufunga mwaka kwa staili ya pekee.
“Hizo surprise nilishaahidi tangu mwanzo na siku zinavyozidi kwenda ndiyo mizuka inazidi kupanda, sitaki kuongea mengi, tukutane Desemba 25 pale Dar Live,” alisema Diamond.

Lakini si umesikia ngoma yake mpya ya Utanipenda aliyoachia Ijumaa ya wiki iliyopita? Basi pata picha inagongwa laivu bila chenga pale uwanja wa taifa wa burudani, Dar Live – itakuwaje?
Ndivyo mchongo ulivyo, Diamond ambaye atapiga shoo hiyo kubwa siku hiyo ya kufunga mwaka 2015 kwenye uwanja huo wa burudani, amepanga pia kutoa surprise special kwa kuitwanga live kwa mara ya kwanza ngoma hiyo kwa ajili ya mashabiki wake watakaojitokeza.

KELELE MITANDAONI

Tangu kuachiwa kwa kichupa hicho, saa chache baadaye, gumzo la kufa mtu liliibuka kwenye makutano ya wengi kule mitandaoni kupitia mitandao ya kijamii kama WhatsApp, YouTube, Facebook, Twitter na Instagram zinakopatikana timu za kila aina, wakieleza kuguswa na mistari na video hiyo iliyotengenezwa na Godfather wa
Afrika Kusini.

Kama hiyo haitoshi, wengi walitamani kumsikia Diamond au Chibu akitwanga ngoma hiyo live na mwisho wa siku ikabainika ni Dar Live pekee ndiyo kuna shoo ya karibu kwa sasa atakayotumbuiza msanii huyo na madensa wake mashuhuri.

MSAGASUMU NAYE

Mkali wa Singeli, Msagasumu anakosa vipi kwenye shoo ya kibabe kama hiyo? Atatia timu na atakamua ngoma zake
zote kali zinazotamba mitaani. Nyimbo kama Inaniuma Sana aliyomshirikisha lejendari Juma Nature, Huyo Mtoto, Shemeji Unanitega, Naipenda Simba na nyingine kibao.

“Wanangu wote tukutane pale Dar Live, itakuwa usiku wetu wote. Ngoma zote kali nitatwanga kama kawa, waje
wengi turuke pamoja, tufurahi,” alisema Msagasumu.

WAKALI DANCERS

Kundi linalosifika kwa sarakasi na kucheza muziki wa kila aina, Wakali Dancers, nalo litakuwa ndani ya nyumba
siku hiyo kukinukisha na kupagawisha uwanja mzima kwa mashabiki watakaojitokeza.

Wametamba kuwa itakuwa si ishu ya kitoto kwani wataonyesha mashabiki mbwembwe zao zote zikiwemo zile
za kujikunjakunja kwa staili kibao na kudansi ngoma za kisasa za ndani na nje ya nchi.

“Sina mengi ya kueleza kuhusiana na shoo baabkubwa tutakayoifanya siku hiyo, michezo yote ya hatari itafanyika siku hiyo, kutoa burudani ndiyo zetu.

Kwa atakayekosa atajilaumu, tutafanya kila kitu kwa ajili ya kufunga mwaka,” walitamba memba wa kundi hilo.

Usisimuliwe sana, tia timu mwanangu uone mwenyewe moto wa burudani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles