28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Bodi ya barabara yakunjua makucha

RFBNa Esther Mnyika, Dar es Salaam

BODI ya Mfuko wa Barabara (RFB) imesitisha kupeleka fedha katika halmashauri tatu nchini zilizobainika kuwa na matumizi mabaya ya fedha hizo.

Zuio hilo lilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Meneja wa RFB, Joseph Haule, mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, wakati akiwasilisha taarifa ya Bodi kuhusu mafanikio na changamoto wakati wa utekelezaji wa kazi.

Alizitaja halmashauri zinazohusika na hatua hiyo kuwa ni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini.

“Baadhi ya halmashauri hizo ikiwamo Kinondoni na Songea Vijijini tumesitisha kuzipatia fedha kutokana na kujenga barabara chini ya kiwango hivyo gharama za marudio ya matengenezo yake watagharamia halmashauri husika.

“Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini iliomba fedha Sh milioni 126 kwa ajili ya matengenezo ya barabara tukawapa lakini zikatumika katika shughuli nyingine,” alisema Haule.

Alisema RFB pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili bodi hiyo imefanikiwa kukusanywa Sh bilioni 752 ambapo asilimia 63 ya mapato hayo ziligawiwa kwa Wakala wa Barabara (Tanroads) huku asilimia saba zikipelekwa Wizara ya Ujenzi na asilimia 30 kwenye halmashauri 166.

Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri Ngonyani alieleza kusikitishwa na matumizi mabaya ya fedha za umma na aliziagiza halmashauri zilizohusika kurudisha fedha hizo.

“Nimesikitishwa na kitendo hiki na naagiza kwamba halmashauri zilizotajwa zihakikishe zinarudisha fedha hizo ili zikatumike katika kazi husika za ujenzi wa barabara,” alisema.

Naibu Waziri huyo aliwataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuajiri wahandisi wenye ujuzi wa kutosha ambao wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Wakurugenzi ajirini wahandisi wenye ujuzi wa kutosha ili matatizo haya yasijirudie kama ilivyotokea kwenye halmashauri hizi,” alisema Naibu Waziri Ngonyani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles