27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Tuliwapenda ila Mungu aliwapenda 2015

bobbi-kristina-b-768NA HASSAN BUMBULI

WIKI iliyopita katika safu hii tulikuandalia habari mbalimbali za wasanii maarufu duniani ambao wanaumaliza mwaka kwa kuonja joto la jela.

Baadhi ya wasanii hao walikuwa wanatumikia kifungo cha muda mfupi, huku wengine wanaonekana wazi kuwa mwaka mpya watauonea gerezani.

Jumamosi ya leo tunakujuza au kukukumbusha vifo vya wasanii mbalimbali ambao wamepoteza maisha mwaka huu.

KRISTINA BROWN

Huyu alikuwa mtangazaji wa vipindi mbalimbali vya runinga, mwanamitindo na msanii wa muziki.
Alitokea katika familia ya muziki ambapo baba yake Bob Brown ni msanii wa Hip Hop, wakati marehemu mama yake Whitney Huston alikuwa mkali wa muziki nchini Marekani.

 

Kristina alifariki dunia Julai 26, mwaka huu katika chumba cha mahututi kwenye Hospitali ya Peachtree Christian Hospice, mjini Georgia nchini Marekani.

Kifo hicho kilitokea baada ya kuugua kwa miezi sita mara baada ya kuanguka bafuni Januari 31, mwaka huu nyumbani kwake Roswell mjini Georgia, ambako alikuwa anaishi na mpenzi wake kwa muda mrefu
Nick Gordon.

Ulikuwa ni msiba ambao uliwashtua watu wengi kutokana na kuugua kwake ambapo alipoteza fahamu tangu siku ya
kwanza anaanguka Januari hadi siku ya kifo chake Julai, takribani miezi sita.

Kifo hicho watu wengi walidai kuwa hakikuwa na tofauti sana na mama yake ambaye alifariki Februari, 2012 baada ya kuanguka bafuni, huku akidaiwa kutumia madawa ya kulevya.

Rita-Anuku-1RITA ANUKU

Alikuwa ni Miss Nigeria mwaka 1986, akijulikana kwa jina la Rita Anuku, ambaye alifariki Julai 4, mwaka huu katika Hospitali ya Abuja nchini Nigeria.

Mrembo huyo kabla ya kupatwa na umauti alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi kwa muda wa miaka miwili.
Rita alianza kuwa maarufu nchini humo huku akiwa na umri wa miaka 18 wakati anasoma elimu ya sekondari, baada ya kumaliza masomo alijihusisha na urembo na kufanikiwa kuchukua taji nchini humo mwaka 1986.

Mrembo huyo alitokea katika familia ya watoto wenye vipaji huku dada yake akiwa mcheza filamu maarufu nchini humo, Hanks Anuku, ambapo familia hiyo ilikuwa jumla na watoto wanne.

SCOTT MARSHALL

Huyu alikuwa mkali wa kuchora michoro mbalimbali kwenye mwili (Tatoo), nchini Marekani, wiki iliyopita alipoteza maisha baada ya kunywa pombe kupita kiasi.
Ink Master Season 4 scott marshallInasemekana kuwa mkali huyo wa michoro, alikunywa pombe ambayo imechanganywa na vinywaji mbalimbali vikali na akapoteza maisha katika hoteli ya IL, jijini Roselle.
Hata hivyo kifo hicho kilileta utata baada ya kukutwa akiwa ametokwa na damu puani na mate mengi mdomoni.

ROSE SIGGINS

Alikuwa mkali wa filamu nchini Marekani, aliwahi kucheza katika Filamu ya ‘America Horror Story’ ambapo alicheza
kama mlemavu wa miguu.
Msanii huyo amepoteza maisha Jumatatu nchini Marekani katika hospitali ya Denver nchini humo baada ya kufanyiwa upasuaji wa figo ambayo ilikuwa inamsumbua kwa kipindi kirefu. Rose amefariki huku akiwa na umri
wa miaka 43, na kuacha watoto wawili. Tuliwapenda, lakini Mungu amewapenda zaidi, walazwe pema peponi – Amen.Rose-Siggins
Tukutane Jumamosi ijayo na vitu vipya vya wasanii kwa mwaka 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles