26.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 16, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond kuanza kupiga ‘live’ Krismasi hii

diamond-numzNa Mwandishi Wetu

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ pamoja na kundi lake zima la Wasafi Classic Baby (WCB), wanatarajia kuanza kupiga ‘live’ kwa kutumia vyombo nyimbo zao zote kuanzia Sikukuu ya Krismasi mwaka huu (Desemba 25) ndani ya Uwanja wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na gazeti hili, Diamond anayetamba kwa wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la Utanipenda, alisema mwaka huu umekuwa na mabadiliko makubwa kwake kimuziki na hatua aliyofikia ni kuupeleka muziki huu kimataifa zaidi.

“Natarajia kupiga ‘live’ kwa kutumia vyombo nyimbo zangu zote kuanzia Krismasi hii pale Dar Live.

“Ujue muziki wetu unatakiwa uendelee kuwa katika ngazi za juu zaidi na ili liwezekane hili inatakiwa tufanye kile wenzetu wanachokifanya,” alisema Diamond.

Diamond ambaye kila kukicha anajizolea tuzo za kimataifa, alisema miongoni mwa nyimbo atakazozipiga siku hiyo ni pamoja na hii ambayo ni habari ya mjini kwa sasa, Utanipenda, Nasema Nawe, Nana, Mdogomdogo na nyingine nyingi.

Mbali na Diamond kuburudisha siku hiyo ya Krismasi, Dar Live, bingwa wa muziki wa Singeli, Msagasumu naye atakuwepo jukwaani kuwapa burudani wapenzi wa muziki huo kwa kupiga nyimbo zake zote kali.

Burudani itashereheshwa pia na mabingwa wa sarakasi na kucheza muziki wa kila aina, Wakali Dancers ambao watakuwepo kukamilisha hamu ya mashabiki wa burudani kwa kuonesha mbwembwe zote za mjini.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles