Mourin kuwafungia kazi Wema, Aunty Ezekiel

0
1279

shostNA HUSSEIN RAMADHAN, TSJ

MSANII anayefanya vizuri katika filamu nchini, Mourin Joseph ‘Mourin’, amepanga kuwafunika baadhi ya wasanii ambao wanafanya vizuri kama vile Wema Sepetu, Aunty Ezekiel, Jacqueline Wolper na wengine wengi.

Mourin alisema alikuwa anavutiwa sana na Aunty Ezekiel, Wema, Rose Ndauke, hivyo ndoto yake ni kufikia mafanikio yao na ikiwezekana kuwazidi.

“Hakuna kisichowezekana, ninachofanya kwa sasa ni kuzidi kujituma na zaidi huwa ninaangalia filamu mbalimbali za wasanii wakubwa hapa nchini na kwingineko ili niweze kujifunza zaidi na kutimiza ndoto yangu ya muda mrefu ya kuwa mchezaji filamu mahiri hapa nchini,” alisema Maourin.

 

Mourin hadi sasa amecheza filamu tano ambazo ni Double J, Second Pain, Kivuli cha Bibi, Upande wa Pili, Joka, Salanja na Masikini wa Kheri, akiwa amefanya kazi na nyota wa tasnia hiyo kama J Plus, Mzee Magali, Bad Boy, Niva, Jengua na Mzee Kankaa ambaye kwa sasa ni marehemu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here