23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

DHAMANA YA LEMA KUJULIKANA LEO

Na JANETH MUSHI, ARUSHA


lemaphotoJAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Fatuma Masengi, leo anatarajiwa kutoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowekwa na mawakili wa Serikali wanaoomba mahakama hiyo isisikilize maombi ya rufaa juu ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema).

Uamuzi huo ndiyo utaamua iwapo rufaa hiyo ya Lema iliyokatwa Novemba 22, mwaka huu chini ya hati ya dharura na mawakili wake, Peter Kibatala, Adam Jabir, Sheck Mfinanga na Rafaji Mangula, itasikilizwa au la.

Rufaa hiyo ilipokelewa mahakamani hapo hivi karibuni na kusajiliwa kwa namba 112 na 113 ya mwaka 2016 na ilitarajiwa kusikilizwa Novemba 28 mwaka huu, lakini ilishindikana kutokana na pingamizi hilo.

Baada ya mawakili wa Lema na mawakili wa Serikali, Matenus Marandu na Paul Kadushi kukutana katika chumba cha ofisi ya Jaji Masengi aliyekuwa asikilize rufaa hiyo, Marandu aliwaambia waandishi wa habari, kwamba wameweka pingamizi hilo kwa kuwa mawakili wa Lema hawakuwasilisha kusudio la kukata rufaa na badala yake walikata rufaa moja kwa moja.

“Tumeweka pingamizi hilo chini ya kifungu cha 361 (1) (a) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

“Baada ya mjadala, tumekubaliana kwa pamoja kuharakisha pingamizi hilo na kuamua lisikilizwe kwa njia ya maandishi,” alisema Wakili Marandu.

Novemba 30, mwaka huu saa mbili asubuhi, mawakili wa Serikali waliwasilisha hoja zao za pingamizi na upande wa utetezi walijibu saa sita mchana na hoja za nyongeza za upande wa Serikali ziliwasilishwa saa tisa alasiri.

Katika rufaa hiyo, mawakili hao wanadai haki ya dhamana ya Lema aliyonyimwa kutokana na makosa ya kisheria yaliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Novemba 8 mwaka huu.

Mawakili wa Lema wanadai kuwa, Hakimu Desderi Kamugisha wakati anasikiliza shauri hilo, alisema mahakama hiyo ingempa Lema dhamana kwa masharti itakayoweka, lakini kabla hajamalizia kutoa uamuzi wake, mawakili wa Serikali walisema wameandaa notisi ya rufaa juu ya uamuzi na hoja hiyo ikaridhiwa na hakimu huyo.

Lema alikamatwa Novemba 2, mwaka huu nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma na hadi sasa yuko katika Gereza la Kisongo mjini hapa kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli kupitia mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali jijini

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles