23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MOROCCO YALALAMIKIA NJAMA ZA KUIZUIA KUREJEA AU

RABAT, MOROCCO


MOROCCO - MOHAMMED VIUFALME wa Morocco umelaani vikali vitendo vya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma, unayeamini anahujumu maombi ya taifa hilo kurejea katika umoja huo.

Mfalme Mohammed VI alitangaza rasmi nia ya Morocco kujiunga tena Umoja wa Afrika (AU) wakati akitoa hotuba nchini Rwanda Julai 17 mwaka huu.

Nchi hiyo ilijitoa kutoka AU miaka 32 iliyopita kupinga kitendo cha chombo hicho kutambua harakati za uhuru wa Sahara Magharibi zinazopiganiwa na vuguvugu la Polisario.

Morocco inasisitiza eneo hilo ni sehemu ya himaya yake.

Ni miezi zaidi ya minne sasa tangu hotuba ya mfalme nchini Rwanda, na ijapokuwa mapema mwezi uliopita Dlamini-Zuma alimuahidi Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar kuwasilisha ombi hilo kwa nchi nyingine za AU, hakuna maendeleo yaliyopigwa hadi sasa.

Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ilitoa taarifa kwamba, “baada ya ucheleweshaji usio na msingi kwa kutosambaza ombi la Morocco kwa wanachama wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma anaendelea kutuhujumu kwa kuweka masharti mapya kinyume na yale yanayofahamika ili ombi letu lisipate baraka kutoka wanachama wa AU.”

“Mwenyekiti wa Tume ya AU anashangaza kwa kushindwa kufanya kazi bila kuegemea upande na kufuata sheria na kanuni za AU na matakwa ya nchi wanachama,” wizara hiyo iliongeza.

“Takriban nchi 36 kati ya 54 wanachama wa AU haziitambui Sahara Magharibi kama eneo huru na ni wakati wa kufuta uamuzi huo,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles