MADRID, Hispania
KOCHA wa waliokuwa mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Vicente del Bosque amesikitishwa na vipigo walivyopata katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
“Kuna vitu vinatokea vinanifanya nitamani kulia, inahuzunisha lakini sina namna nyingine natakiwa kukubaliana na yote. Mimi ni mwana michezo na hakuna kitu kinachouma kama kufungwa. Natamani tungendelea na mashindano, Kombe la Dunia limejaa maajabu ni mashindano yanayochanganya akili,” alisema Del Bosque.
“Tumeshutumiwa sababu tumecheza hovyo mechi zetu mbili za mwanzo za Kombe la Dunia. Sifa zote zimeenda kwa Uholanzi na Chile.”
Kocha huyo aliisaidia Hispania kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2010 pamoja na kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012. Licha ya kutolewa mapema, chama cha soka nchini Hispania kimesema ataendelea na kibarua chake.