29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Barca yamng’ang’ania Luis Suárez

Luis Suarez
Mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez

Suarez-bite-1BARCELONA, Hispania

MIAMBA ya soka nchini Hispania, klabu ya Barcelona imesisitiza kuwa na mpango wake wa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay, Luis Suarez licha ya kutuhumiwa kumng’ata begani beki wa Italia, Giorgio Chiellini.

Nyota huyo anafukiziwa ili awe sehemu ya kikosi kipya kinachosukwa na kocha mpya wa Barcelona, Luis Enrique, ambaye amewaambia viongozi wake wafanye kila wanaloweza ili kumsajili staa huyo.

Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amethibitisha kutobadili mipango ya kumsajili Luis Suarez, akilazimika kushindana na Real Madrid ili kumnasa mshambuliaji huyo wa Liverpool.

Barca imeandaa Euro milioni 87.5 ili kumsajili Suarez pamoja na kuwapa mchezaji Liverpool kati ya Alexis Sanchez, Pedro Rodriguez, Cristian Tello au Alex Song.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles