Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM
JUMATATU jioni wiki iliyopita Daniele De Rossi alihoji ombi la kocha wake la kumtaka ajiandae kuingia uwanjani wakati timu yao ya taifa ya Italia ilipokuwa ikijitutumua kuokoa matumaini yao ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika Urusi mwakani.
Lakini katika hali hisiyo ya kawaida alionekana kuwa mkali huku akitaka aingie mshambuliaji wao Lorenzo Insigne, badala yake huku akimkumbusha kocha wake wa viungo kwamba walikuwa wanahitaji kushinda, si kupata matokeo ya sare.Akifaham kwamba nafasi ni kukaba si kushambulia.
Naamini kile ambacho De Rossi alifanya ilikuwa kitu ambacho kwa wakati fulani kila mchezaji duniani huhisi kufanya.
Nimehisi hasira ya De Rossi, kuchanganyikiwa kwa kuangalia timu yake ikipambana wakati ameketi kwenye benchi na najua maumivu na hisia za mchezaji kutokuwepo uwanjani haziwezi kubadilisha matokeo ya mechi muhimu.
De Rossi anasema: “Nilikwenda chini kuzungumza na kumpigia kelele kocha kufanya mabadiliko ingawa hisia hiyo ni ngumu sana na ngumu kuelezea ni ya asili hata hivyo ni ishara nzuri kwa maana ina maana mimi najali.”
Ningeweza tu kufikiri jinsi gani De Rossi, mchezaji wa kiungo mkabaji, alivyokuwa akijisikia wakati akiangalia nafasi yake ya mwisho ya kujigamba akiwakilisha taifa lake katika Kombe la Dunia ikipotea.
Kawaida mchezaji anahisi kuchanganyikiwa kwa hasira wakati anapokuwa hayupo kwenye kikosi cha kwanza au kuingia badala ya mchezaji mwingine tabia hii inaitwa ubinafsi ambayo wachezaji wengi wanayo lakini hilo halikuonekana kwa De Rossi.
Kinachofanya kitendo cha De Rossi kuwa hadimu ni ile hali ya kuashiria mchezaji mwingine aingie uwanjani badala yake, ni kwamba ilikuwa ishara ambayo ilionyesha kuwa alijali zaidi manufaa ya timu yake kuliko binafsi.
Baada ya Italia kuondolewa na Sweden, kufuzu Kombe la Dunia, kocha wa Ujerumani, Joachim Löw, alielezea kitendo cha De Rossi kama “wakati wa ukuu”.
Ninaelewa wapi ametokea lakini ni kweli Löw angevumilia kama kitendo kile angekifanya moja ya wachezaji wake kwa kumkosoa kimbinu mbele ya umati, ingekuwaje? Sidhani kama angevumilia.
Ni kama ncha ya upanga ambayo huelekea kwa wachezaji na makocha, ninaelewa na kuhisi kitendo vya De Rossi lakini kuwa kama mchezaji si tu anawajibu wa kushinda kila kitu, kujali timu na kusapoti wachezaji wengine lakini pia wana wajibu wa kumheshimu kocha wao hadharani, kwa kuwa ndio aliyepatiwa madaraka ya kufanya maamuzi ya timu.
Kuna wakati makocha wangepingwa sana kutokana na maamuzi yao na kuweza kumuuliza”Unafikiri nini kwa mabadiliko haya?”.
Ni swali linalopatikana wakati wanapofanya uamuzi ambao haukubaliki na baadhi ya wachezaji au mashabiki walioko uwanjani lakini jambo hilo halitokei labda kwa uwoga au kumuheshimu.
Inawezekana jambo hilo likawa tofauti zaidi ya taaluma nyingine yoyote, kwani mchezo wa soka unapaswa kuwa na maoni na imani ya karibu kwa kila mtu aliyekaribu na mchezo huo, lakini mchezaji anaweza kufikiri hali ya mchezo kabla ya kutakiwa kuingia uwanjani na kujaribu kujadili umuhimu wake kwa timu au kufanya uamuzi tofauti wa kimbinu? Sidhani.
Mashirika ya uma na binafsi, biashara na klabu za soka zote zina mawazo tofauti katika muundo wa uongozi wenye nguvu.
Baadhi wanajumuisha zaidi katika mchakato wa kufanya maamuzi na wengine ni wa kidemokrasia tu, bila ya kuingia katika faida na hasara ya kila aina ya mtindo wa uongozi, lakini katika soka, huku ni mtu mmoja tu ambaye huwapa faida au hasara.
Hakukuwa na mshtuko kwamba kocha wa timu ya taifa ya Italia, Gian Piero Ventura angefukuzwa na Chama cha Soka cha Italia (FA), kwa kuzingatia ilikuwa mara ya kwanza kutofuzu wakati mchezo wa soko ukiwa katika umiliki wa kizazi kipya.
Ingawa alifukuzwa, kwa kweli aliangukia nchi ya upanga kutokana na uamuzi wake wa kushindwa kumuingiza Insigne, pamoja na yote aliyofanya ikiwamo maelekezo ya kimbinu.
Jambo ambalo De Rossi alifanya ni shauku, uzalendo kwa mtazamo wake kwa maslahi ya timu yake. Kwa hiyo hakuna shaka.