26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

DC Sengerema aonya watakaokaidi kushiriki shughuli za maendeleo

Na Anna Ruhasha, Sengerema

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Senyi Ngaga amewatahadharisha wananchi watakaokaidi kushiriki shughuli za maendeleo husasan katika miradi iliyoelekezwa michango ya nguvu za wananchi kuwa watakuwa mfano kwa wawengine.

Sehemu ya wananchi.

Ngaga ametoa onyo hilo juzi wakati akizindua mradi wa ujenzi wa kituoa cha afya katika kijiji cha Kanyelele kilichopo kata ya Buzilasoga Halmshauri ya wilaya ya Sengerema mkaoni hapa.

Mradi huo unatekelezwa na wananchi kupitia mradi wa Tasaf ambapo unatarajiwa kugharimu Sh milioni 500.

‘’Kwanza ni washukuru wananchi wa kata hii kwa ujumla nimeona tayari mmeshajitoa kuchangia mawe na mchanga kwani kila mradi unakuja na masharti yake na huu wa TASAF ulikuja na mwongozo wa jamii ichangie nguvu kazi siyo pesa.

“Kama mlivyofanya ninyi hapa, tayari tumeishapokea zaidi ya Sh milioni 300 za ujenzi huu, hivyo nikuagize mtendaji kwa wale watakaokaidi kushiriki nilitee wawaili tu watakuwa mfano,” amesema Nganga.

Ameongeza kuwa matumaini yake ni kuona mradi huo unasimamiwa kwa ubora na unakamilika kwa wakati ili adhima ya serikali kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya afya katika kata hiyo inatimia kama ilivyokusudiwa.

Aidha, mtendaji wa kata hiyo, Elizabeth Amoni katika taarifa yake amesema mwitikio wa wananchi ni mzuri ambapo jumla ya tripu 50 za mawe na 11 za mchanga zimeishakusanywa kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo akiwamo, Rehema Philipo amesema kujengwa kwa kituo hicho kutasaidia kuondoa changamoto ya wagonjwa kutumbea umbali wa zaidi ya kilometa 20 ambapo walikuwa wakipata huduma hiyo Sengerema mjini na mkoa jirani wa Geita.

Kwa upande wake mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Nduga Malisa ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2021 \2022 Tasaf kwa kushirikiana na wananchi wameibua miradi 15 ukiwemo ujenzi wa kituo cha afya Kanyelele, nakwamba kwa mradi huo wa wananchi watagharamia kwa asilimia 100.

“Mradi huu unahusisha majengo matatu ya Maabara, jengo la wagonjwa wa nje na lile la mama na mtoto,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles