24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

DC Mbulu awataka wananchi kuziunga mkono taasisi za kifedha

Na Mwandishi Wetu, Manyara

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Dk. Chelestino Mofuga amewataka wananchi kuziunga mkono Taasisi za kifedha zinazoshirikiana nao katika kuihudumia jamaii.

Dk Mofuga alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwenye hotuba yake alipokuwa akipokea msaada wa mshuka, vitanda na magodoro  yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili hospitali mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara iliyopo eneo la Dongobesh .

Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuziunga mkono taasisi  zinazotoa huduma za kifedha  ambazo zipo tayari kuendelea kushirikiana na Jamii kwa kutoa misaada.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Dk. Chelestino Mofuga (kushoto) akiwa na Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hatson Kamoga (wapili) pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo, Flatei massay (watatu) wakipokea msaada wa mashuka 25 na vitanda 8 na magodoro yake kutoka kwa Meneja wa Nmb Tawi la Mbulu, Adamu Mwaisumo (kulia).

“Na hapa naomba niwe mkweli tangu nimekuja hapa nasikia benki ya  Nmb wanakabidhi misaada maeneo mbalimbali wilayani hapa, na leo nimepokea  msaada mwingine hawa ndio watu mnaotakiwa kuungwa mkono kwa sababu wanarudisha faida kwenye jamii yetu na tunaiona,”alisema.

Aliongeza kuwa benki ya NMB imekuwa ni taasisi pekee ya kifedha inayotoa huduma za kifedha kwa  kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya vijijini bila kujali faida kama wengine wanaonga’ng’ania mijini.

Aidha, aliwataka wananchi kutumia taasisi za kifedaha katika kuhifadhi fedha zao ili kuepuka kupata hasara wakati wa majanga ya moto au wizi kwenye nyumba zao .

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya aliahidi kuwa balozi wa benki ya NMB nchini kwa kuisemea kutokana na misaada inayotolewa katika maeneo mbalimbali inavyoigusa jamii.

Naye, Meneja wa NMB Tawi la Mbulu, Adamu Mwaisumo alisema  benki hiyo imekabidhi mashuka 25, magodoro nane na vitanda nane kwa ajili ya wodi za kawaida na akinamama kujifungulia ya hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu iliyopo mKoani Manyara

Mwaisumo alibainisha kuwa msaada huo wa vifaa hivyo vyote unathamani ya shilingi milioni tano ambazo zimetokana na asilimia 1 ya faida baada ya kodi inayotengwa na NMB kila Mwaka katika kuirudisha kwenye jamii.

Alisema benki hiyo inasaidia jamii katika sekta ya elimu kwa kuchangia madawati,viti na meza pamoja na kusaidia kuezeka majengo mapya ya shule au nyumba za waalimu

Aliongeza kuwa eneo lingine ambalo NMB inasaidia jamii kuwa ni sekta ya afya kwa kutoa vifaa tiba,mashuka,magodoro,vitanda vya kawaida na akinamama  kujifungulia

Pia alisema lengo la msaada huo wa Nmb ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli katika kuihudumia jamii.

Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbulu, Hardson Kamoga alisema hospitali hiyo mpya inakabiliwa na changamoto ya vifaa hivyo anaziomba Taasisi zingine kujitokeza kusaidia.

Aliwashukuru benki ya NMB kwa msaada uliotolewa na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa ili kuendelea kuwasidia wananchi wote wanaofika kupata huduma hapo .

Alibainisha kuwa hospitali hiyo mpya imeanza kutoa huduma za awali lakini bado huduma hivyo wananchi wafike kupata huduma za kiafya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles