23.1 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC Magoti ajipanga kuwanyanyua wajasiriamali

Na Elizabeth Zaya, Dar es Salaam

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, amesema wamejipanga kuwasaidia wajasiriamali katika wilaya hiyo ili wafanye biashara za viwango vya juu.

Magoti alitoa kauli hiyo jana alipotembelea maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Temeke.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe(mwenye suti nyeusi) Petro Magoti akizungumza na Wajasiriamali kwenye maonesho ya sabasaba, viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa, Temeke

Alisema Kisarawe ni miongoni mwa Wilaya yenye bidhaa nyingi hivyo ni vema kutumia wajasiriamali hao ambao wamekuwa wakiendesha biashara kupitia bidhaa hizo kuwainua na kuzitangaza zaidi.

“Kisarawe ni moja ya wilaya inayotengeneza bidhaa nyingi ikiwamo wine inayoitwa Chole, tunatengeneza kwa kutumia mabibo, tuna Zabibu na Korosho ambayo inavitamini yote, kwa hiyo sisi kama viongozi wa wilaya hii, tumejipanga kuwasapoti wajasiliamali ili wafanye biashara kufikia ngazi ya juu,”alisema Magoti.

“Kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoagiza kwamba wajasiriamali wapate maeneo maalum ya kufanyia biashara zao, na sisi viongozi wa wilaya hii tuliona tuje kuangalia na kujifunza kutoka kwenye mikoa mbalimbali ndani na nje ya nchi wanaoshiriki kwenye maonesho haya ili tukirudi tuweke mipango mizuri ya kuwasaidia wajasiriamali wa wilaya hii”

Kuhusu maonesho ya mwaka huu, Magoti alisema kuna mabadiliko makubwa katika kila eneo kwenye maonesho hayo.

“Kadri siku zinavyokwenda maonesho yanazidi kuwa makubwa na mazuri na mataifa mengi yanazidi kushiriki, tunaamini kwamba zile changamoto ndogondogo zitazidi kupungua na uwezeshwaji wa wananchi wengi kushiriki utazidi kuongezeka,”alisema Magoti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles