27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC Ludigija ataka usimamizi ujenzi vituo vya afya

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija, amezitaka kamati za ujenzi kusimamia vema ujenzi wa vituo vya afya ili kuwe na miundombinu yenye ubora na inayokidhi thamani ya fedha.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija, akizungumza baada ya kukagua jengo la wagonjwa wa dharura linalojengwa katika Hospitali ya Jeshi Magereza. Wanne kushoto ni Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Abdilatif Mkingule na Kulia ni Diwani wa Kata ya Ukonga, Ramadhani Bendera.

Ludigija ameyasema hayo baada ya kufanya ziara kukagua ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za Kipunguni, Majohe pamoja na jengo la wagonjwa wa dharura linalojengwa Hospitali ya Jeshi la Magereza.

Kituo cha Afya Kipunguni kinajengwa kwa fedha za tozo wakati kile cha Majohe kinajengwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri na jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Jeshi Magereza linajengwa kwa fedha za Uviko – 19.

Katika Kituo cha Afya Majohe Ludigija hakuridhika na mawe yaliyokuwa yamemwagwa katika jengo la upasuaji kwani hayakidhi viwango na kuagiza yaondolewe yawekwe mengine.

“Hili jengo la upasuaji ambalo lipo hatua ya kumwaga jamvi mawe yake hayakidhi viwango, si yale yanayotakiwa kutumika kwa jamvi, aliyeleta aagizwe kama anashindwa atafutwe mtu mwingine yaletwe mawe mengine,” amesema Ludigija. 

Akikagua jengo la wagonjwa wa dharura Hospitali ya Jeshi la Magereza amesema ameridhishwa na ujenzi huo na kusema hana wasiwasi na jeshi hilo katika usimamizi wa miradi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Jeshi la Magereza, Dk. Abdilatif Mkingule, amesema walipokea Sh milioni 300 ambapo ujenzi ulianza Februari 6 na unatarajiwa kukamilika Aprili 30.

Aidh katika kituo cha afya Kipunguni Ludigija ameitaka kamati ya ujenzi kuhakikisha wanakamilisha majengo kwa wakati ili waweze kuingiziwa fedha nyingine za kukamilisha kituo hicho.

Naye Diwani wa Kata ya Kipunguni, Steven Mushi, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowezesha kata hiyo kupiga hatua kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo hicho, maradasa 17 ya sekondari na ukarabati wa barabara kuu kwa kuchongwa na kuwekwa vifusi.

Amesema pia wamepokea Sh milioni 40 za ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Kipunguni ili kupunguza msongamano pamoja na Sh milioni 20 za ujenzi wa matundu ya vyoo.

Diwani huyo pia amemuomba mkuu huyo wa wilaya kuwasaidia kukarabati barabara inayoingia katika kituo hicho cha afya na suala la urasimishwaji ardhi kwani ndio kilio kikubwa kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles