27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

DC James aitaka jamii kushirikiana na walimu katika malezi

Na Asha Bani, Mtanzania Digital

Mkuu Wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James ameitaka jamii kushirikiana na walimu katika malezi bora ya watoto ili kulinda maadili yao.

James ameyasema hayo Septemba 28, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na walimu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Asante Mwalimu’ katika kuelekea  maadhimisho ya siku ya mwalimu Duani.

Picha ya pamoja.

Amesema jamii ilimkubali mwalimu toka zamani na ndio maana kuna ushirikiano huku akisisitiza wazazi kuendelea kuwa na ushirikiano nao katika kujadili maendeleo ya watoto. 

Akizungumza kuhusu benki ya walimu amesema ni mkombozi wa kwani walimu wengi walikuwa wakijiingiza kwenye mikopo isiyo rafiki kwao na kuwafanya kuwa na madeni yasiyokuwa ya lazima.

Alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha fedha  zinazunguka kwa wafanyabiashara hivyo aliwataka walimu kuitumia vyema benki hiyo ili  kujikwamua  na maisha.

Mkuu wa Kitengo cha biashara wa benki hiyo, Leticia Ndogole alisema Mwalimu Benki imezindua kampeni ya ‘Asante Mwalimu’ikiwa na dhumuni kuelekea maadhimisho ya siku ya Mwalimu duniani na kuunga mkono  juhudi za serikali katika kuhakikisha walimu wanakua na mazingira bora kwenye utani huduma kwa jamii na hata baada ya utumishi wao.

Alisema kupitia kampeni hiyoMwalimu benki wanatambulisha bando la mwalimu ambao ni mkusanyiko wa bidhaa mbalimbali zinazomlenga mwalimu moja kwa moja nikiwa na lengo la kumpata suluhisho la kifedha .

“Pia kumlinda mwalimu na athari kubwa za mikopo umiza ambayo imeendelea kuwa kilimo kikubwa kwa walimu nchini.

“Bando la mwalimu kama nilivyosema  awali ni mkusanyiko wa bidhaa mbalimbali ambazo unaenda sambamba na safari ya maisha ya mwalimu,” amesema Leticia. 

Ameselisema kuwa mwalimu benki itaanza na mwalimu toka akiwa mwanafunzi alisoma walimu alipoanza kazi,maisha yake ya ajira kwa ujumla anapojotayarisha kustaafu na maisha baada ya kustaafu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles