22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

DC Ileje awaonya watendaji wazembe

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya amewaonya watendaji wa kata na Halmashauri wanaofanya kazi kwa mazoea na kusababisha kukwamisha shughuli za maendeleo kinyume na matakwa ya Serikali na kusisitiza kuwa hatawavumilia.

Gidarya ametoa kauli hiyo Februri 8, 2022 wakati wa kikao na Wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali kilichohusu kutoa mwelekeo wa serikali katika kuwatumikia wananchi.

Akizungumzia mienendo ya Maafisa Watendaji Kata, Gidarya amesema baadhi yao hawafanyi kazi kwa kuzingatia suala la Utawala Bora na matakwa ya serikali inayolenga kupunguza kero kwa wananchi hususan kusimamia miradi ya maendeleo na kwamba viongozi wa namna hiyo hawatavumiliwa.

“Wasimamizi wa miradi ya maendeleo wanapaswa kuendana na kasi ya serikali na kwa viwango vinavyotakiwa pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa wakati sambamaba na thamani ya miradi kuendana na fedha iliyotolewa na serikali amesema Gidarya”.

Gidarya amewashukuru watendaji waliopewa dhamana ya kukusanya na kusimamia mianya ya kukwepesha mapato hivyo kuwataka kazi hiyo kuwaendelevu ya ukusanyaji wa mapoto hususani watendaji wa serikali, viongozi wa siasa na wananchi kwa ujumla kwa kuondokana na kushika mkia kimkoa  kwa halmashauri zote tano za Songwe.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa idara na vitengo afisa kilimo wa wilaya ya Ileje, Herman Njeje amempongeza mkuu wa wilaya kwa kikao hicho cha pamoja ambacho amesema kimesaidia kujua namna bora ya kuwahudumia wananchi kwenye Awamu hii ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles