Dayna: Hakuna mpinzani wa Kanumba

0
2452

Kanumba (61)_595NA JUMA HEZRON, TSJ
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dyana Nyange ‘Dayna’, amesema hadi sasa hakuna mwigizaji wa filamu ambaye ameweza kufikia kiwango cha marehemu Steven Kanumba.
Akizungumza na MTANZANIA leo, Dayna alisema tangu kufariki kwa Kanumba, tasnia ya filamu imebadilika na kuwa ya kawaida sana.
“Hakuna aliyeweza kufikia kiwango cha Kanumba, licha ya wengi wao kujituma na kujitahidi kufanya kazi na wasanii kutoka nje ya nchi,” alisema Dayna.
Mwanadada huyo aliendelea kusema ni vizuri waigizaji wakajipanga upya kuonyesha ushirikiano ili kuhakikisha tasnia hiyo inafika mbali na kufanya vizuri kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here