Dawa bandia zabainika katika vituo vya afya Musoma

0
1217

7

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Ofisi ya Kanda ya Ziwa imebaini kuwapo dawa bandia katika maduka ya kuuza dawa na vituo vya afya katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Mkaguzi wa Dawa wa TFDA, Mtani Njegere alisema baadhi ya maduka yalikutwa na dawa bandia na nyingine ambazo hazijasajiliwa TFDA hivyo ubora na usalama wake kutofahamika yakiwamo makpo 39 ya praziquantel 600mg.

Naye Mkaguzi Mwandamizi wa Chakula wa TFDA, Julius Panga alieleza katika ukaguzi huo zilibainika bidhaa ambazo hazina usajili wao hivyo ubora na usalama wake kutofahamika ikiwamo chumvi ya kaysalt premium inayotengenezwa Kenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here