28.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

Kituo cha uokoaji Ziwa Victoria kujengwa Mwanza

Mwanza

Kituo kikubwa cha Utafutaji na Uokoaji Majini (MRCC) kitakachotoa huduma kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri wa majini ndani ya Ziwa Victoria kinatarajiwa kujengwa Mwanza.

Hayo yalielezwa na Mtaalamu wa Masuala ya Usafiri wa Majini kutoka Kamisheni ya Ziwa Victoria (LVBC) Makao Makuu Kisumu Kenya,Gerson Fumbuka.

Alisema kituo hicho ambacho kinatarajiwa kuanza kujengwa mwezi ujao katika bandari ya Mwanza kwa ushirikiano wa LBVC na Benki ya Afrika kitatoa huduma ya uokoaji ndani ya ziwa na visiwa vyake.

Aliongeza kuwa mradi huu utahusisha pia boti za uokoaji zitakazotoa huduma hiyo inakapohitajika katika nchi zinazotumia Ziwa Victoria na utaweza kutumiwa na maziwa yote nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles