25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Darasa la saba kuanza mitihani kesho

Na Juliana Samwel, TUDARCo

JUMLA ya wanafunzi 1,132,143 katika shule 17,585 nchini kesho wanatarajia kuanza mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi (PSLE) kwa mwaka 2021.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania,  Charles Msonde, watahiniwa waliosajiliwa ni  1,132,143, kati yao wavulana ni 547,502 sawa na asilimia  48.36 na wasichana ni 584,641 sawa na asilimia 51.64.

Amesema kati ya watahiniwa 1,132,143 waliosajiliwa kufanya mtihani mwaka huu, 1,079,943 sawa na alisilimia 95.39 watafanya mtihani wa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 52,200 ambayo ni asilimia 4.61 watafanya kwa Kiingereza, lugha ambazo walikuwa wanazitumia katika kujifunza.

Aidha, amesema watahiniwa wenye mahitaji maalum wapo 3,327, kati yao 108 ni wasioona, 951 wenye uoni hafifu, 739 wenye uziwi, 358 ni wenye ulemavu wa akili na wenye ulemavu wa viungo vya mwili ni 1,171.

Msonde amesema kuna ongezeko  la watahiniwa 101,193(10.57%) kwa  mwaka 2021 ulikinganishwa na mwaka 2020.

“Katika  mtihani huu, idadi ya masomo imeongezeka kutoka matano yam waka 2020 na kuwa sita, somo lililoongezeka linaitwa Uraia na Maadili. Maboresho hayo yamezingatia utekelezaji wa mtaala unaotumika kwa watahiniwa tangu walipoanza masomo yao.

“Pia masomo mawili yameboreshwa maudhui yake hivyo somo la Sayansi litaitwa Sanayansi na Teknolojia na somo la Maarifa ya Jamii litaitwa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles