24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dar yajipanga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi

Na Christina Gauluhanga, Mtanzania Digital

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imesema limejipanga kuhakikisha inaongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwafikia wale wenye mahitaji maalum ili waweze kunufaika na elimu hiyo.

Baadhi ya walimu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakifurahia tuzo zilizotolewa na Halmashauri hiyo kwa ajili ya kutambua mchango wap Katika sekta ya elimu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 2, 2022 katika hafla ya utoaji tuzo kwa Shule za Msingi za serikali na Binafsi 20 sambamba na walimu wakuu waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa, Ofisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo, Sipora Tenga amesema, ili kukamilisha mpango huo hadi sasa wametenga shule 15 za Serikali na vituo ambavyo vimekuwa vikitoa elimu kwa watu wenye mahitaji maalum.

Amesema mpango mkakati huo utawasaidia kupanda kielimu kutoka kiwango cha ufaulu cha sasa ambacho Halmashauri hiyo imekuwa namba nne kitaifa na ya pili kimkoa..

Ametaja shule zinazotoa elimu kwa wenye mahitaji maalum ni Mtemdeni,Msimbazi Mseto, Mzambarauni, Buguruni Viziwi Uhuru Mchanganyiko, Maarifa, Pugu Kajiungeni, Air Wing, Chanika, Viwege na Tumaini.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, N’gwilabuzu Ludigija akitoa vyeti na tuzo kwa walimu na Shule zilizogajua vizuri Katika mitihani ya kitaifa ambapo Halmashauri ya Jiji Ilala iliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya nne kitaifa na ya pili kimkoa.

Kwa upande wa vituo vinavyotoa huduma kwa wanafunzi wagonjwa waliopo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mahabusu ya Watoto iliyopo Upanga na wanafunzi wenye magonjwa adimu waliopo nyumbani.

“Katika kutekeleza mkakati huu wa ufaulu na kuwafikia wanafunzi wenye mahitaji maalum kielimu tumepanga walimu ambao wamekuwa wakiwafuata huko walipo na tumeona mafanikio mmoja wa wanufaika hao amefaulu kwa kiwango cha juu kitaifa,” amesema Sipora.

Amesema Halmashauri hiyo inaendelea na uandikishaji wanafunzi wa darasa la kwanza ambapo hadi kufikia Machi 31 Mwaka huu watakamilisha uandikishaji ambapo kwa sasa 25,695 tayari wameandikishwa.

Amewapongeza walimu hao kwa kuongeza kiwango cha ufaulu ambapo asilimia ya ufaulu imekuwa ikiongezeka Mwaka hadi Mwaka.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, N’gwilabuzu Ludigija aliwapongeza walimu hao kwa ufaulu huo na kuwaagiza waendelee kushirikiana kwenye changamoto ili kuzidi kuinyanyua kielimu halmashauri hiyo.

Amesema wamefanya jitihada za kutengeneza miundombinu kadhaa ya kielimu ili kurahisisha utendaji kazi na hatimaye kunyanyuka kidedea kwenye mitihani mbalimbali.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Ilala, Tabu Shaibu, amewapongeza walimu hao kwa ufaulu wa matokeo yaliyopita na kusema yameenda sambamba na hadhi ya eneo husika.

Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya shughuli hiyo, Godrick Rutayungururwa amesema, tuzo hizo zimetolewa kama motisha kwa walimu hao ili kuinua chachu ya ufundishaji zaidi ambao utanyanyua kiwango cha elimu nchini.

Amezitaja baadhi ya tuzo hizo kuwa ni uongozi, Sanaa na michezo, taaluma na utendaji wa heshima.

Rutayungururwa amesema kumetolewa tuzo kwa shule za msingi Serikali 10 zilizofanya vizuri na shule 10 binafsi.

Pia amesema tuzo nyingine 36 zimetolewa kwa Maafisa elimu kata na Walimu wakuu tuzo 248 kutoka shule zilizofanya vizuri katika upimaji darasa la nne na la saba.

“Tuzo nyingine 23 zimekwenda kwa mdhibiti ubora wa shule na umitashumita,
tano kwa nyingine Walimu ambao wanafundisha watoto wenye mahitaji maalumu katika hospitali ya Taifa Muhimbili, mahabusu ya watoto na mtoto mwenye tatizo la kiafya anayefundishwa nyumbani.

Aliongeza kuwa tuzo nyingine zimetolewa kwa idala mbalimbali ikiwemo madereva wa idara tuzo tano, kamati ya huduma ya jamii na uchumi tuzo moja, Afisa elimu mkoa moja, Naibu Meya moja, Mkurungezi , Meya na ofisi nyinginezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles