30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

TRA yawataka wafanyabiashara Kagera kukaa mguu sawa

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Wafanyabishara mkoani Kagera wametakiwa kukaa tayari kwa ajili ya kuanza kutumia mfumo mpya wa uwasilishaji wa kielekroniki wa ritani ya VAT inaotarajiwa kuanza mapema mwezi huu.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Huduma wa TRA Mkoa wa Kagera, Alex Mwambenja wakati akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba namna ya kutumia mfumo huo utakao saidia kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo wafanyabishara kupigwa faini pindi wanapochelewa kulipa kodi.

“Nitumie fursa hii kuwaomba wafanyabiasha kuwa na kompyuta ambazo zinatumia mfumo wa ‘Excel’ ya kuanzia 2010 hii itawasaidia kuwasilisha ritani kwa usahihi zaidi, tunawakumbusha pia kuwasilisha makadilio yenu yote ya mapato kabla yaMachi 31, mwaka huu ili kuepusha faini ambazo sio za lazima,” amesema Mwambeja.

Amesisitiza kuwa, wafanyabishara wote hasa wale wanaofanya biashara kutoka nje ya nchi wahakikishe wanapoenda kununua bidhaa wawekewe TIN zao wakati wa manunuzi.

“Mfanyabiashara yoyote ambaye hatawekewa TIN yake pamoja na namba ya kudhibitisha wakati wa manunuzi ya bidhaa yake, lisiti hiyo aitatumika kwenye madai ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT),” amesema.

Kwa upande wake, Ibrahimu Sokwala ambaye ni mfanyabiashara katika halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, ameishukuru TRA mkoani Kagera kwa utoaji wa elimu juu ya mfumo mpya wa kielekroniki wa uwasilishaji wa ritani ya VAT na kuiomba mamlaka hiyo kuendelea kutoa semina kama hizo kwa wafanyabiashara kwani zinawasaidia kuongeza uelewa.

“Mimi mlipa kodi nimefurahi sana tunapopatiwa semina kama hizi, mfano wafanyabiashara wengi kabla ya kupatiwa elimu juu ya mfumo huu mpya unaoenda kutumika tulikuwa tunajiuliza maswali mengi hasa kama tutaweza kuumudu lakini kupitia semina hii ambayo tumepatiwa tumejifunza na kupatiwa majibu ya maswali mbalimbali ambayo yalikuwa ya kitu kwaza” amesema Sokwala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles