24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

DAKTARI: KUKOJOA KITANDANI KUNATIBIKA

Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

 

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya akili kwa watoto na vijana wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Doroth Mushi, amesema tatizo la kukojoa kitandani kwa watu wazima linatibika.

Akizungumza na MTANZANIA hospitalini hapo hivi karibuni, Dk. Mushi alisema wamekuwa wakipokea vijana mbalimbali wanaokabiliwa na tatizo la kutokwa na haja ndogo kitandani wakiwa usingizini na kuwapatia matibabu.

“Vijana wenye tatizo hili ni wengi, hasa wale waliofikia umri wa kuoa au kuolewa, huwa wanakuja hapa tunawatibia. Kuna dawa huwa tunawapatia, lakini pia tunawapa ushauri nasaha,” alisema Dk. Mushi.

Alisema Idara ya Magonjwa ya Akili hospitalini hapo ndiyo inayohusika kutoa matibabu ya tatizo hilo ambalo linatajwa kuwa lipo katika kundi la magonjwa ya akili.

“Kukojoa kitandani ni tatizo la kiakili, kawaida tatizo huanza kujitokeza wakati wa ukuaji wa mtoto, lakini kwa kuwa wengi hawajui, huchukulia kama ni hali ya kawaida na kwamba litaisha kadiri anavyoendelea kukua,” alisema.

Alisema ingawa wapo ambao huacha kukojoa kitandani bila kwenda hospitali, wengine hali hiyo huendelea nayo hadi wanapofikia umri wa ujana kwa kukosa matibabu mapema.

“Kwa sababu wazazi wengi hawajui kwamba ni tatizo la akili, mtoto akiendelea kupatwa na hali ya kutoa haja ndogo kitandani mara kwa mara na wapo ambao hutoa hata haja kubwa, huishia kuwaadhibu badala ya kuwafikisha hospitalini kwa uchunguzi na tiba,” alisema.

Alisema ni kweli wazazi wanayo haki ya kuwaadhibu watoto na vijana wao, lakini hiyo si tiba sahihi, hivyo wanapaswa kuwafikisha hospitalini iwapo hali hiyo inajitokeza mara kwa mara.

Daktari huyo ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), alisema zipo sababu nyingi zinazochochea mtoto kupata matatizo ya akili, ikiwamo mjamzito kukaa na uchungu kwa muda mrefu.

“Matatizo ya akili mengine hurithiwa kwa sababu yapo kwenye vinasaba. Pia mtoto hupata tatizo iwapo mama akikaa na uchungu muda mrefu wakati wa kujifungua, hali hiyo husababisha athari kwenye ubongo wa mtoto, kwani hukosa oksijeni ya kutosha,” alisema.

Aliongeza kuwa yapo pia baadhi ya magonjwa ambayo mama akiugua katika kipindi cha ujauzito huweza kumsababishia mtoto athari katika ubongo wake, ndiyo maana wataalamu wa afya husisitiza mama afike kliniki kipindi chote cha ujauzito.

 

Kwa kujua sababu nyingine nyingi zinazosababisha kukojoa kitandani na jinsi ya kumtambua mtoto mwenye tatizo hilo, soma makala ukurasa wa vi-vii katika Jarida la Afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles