24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

CUF: Vikao vitaamua barua ya Lipumba

Profesa Ibrahim Lipumba
Profesa Ibrahim Lipumba

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimewataka wanachama wake kusubiri uamuzi wa vikao kuhusu hatima ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Profesa Lipumba aliyetangaza kuachana na uongozi wa CUF, Agosti 8 mwaka jana baada ya chama hicho kukubaliana na Ukawa kumsimamisha Edward Lowassa kuwania urais, ameomba tena juzi kurejea kwenye wadhifa wake.

Kutokana na uamuzi huo wa Profesa Lipumba, kumekuwa na taarifa kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif amekataa uamuzi huo akimtaka atafute uenyekiti sehemu nyingine.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Salim Bimani, ilisema kuwa Maalim Seif hajatoa msimamo wowote na kwamba yuko Marekani.

“Maoni na msimamo wa Katibu Mkuu, Maalim Seif ambaye yuko Marekani ni kwamba wanachama wasubiri maamuzi ya vikao vya chama vitaamua mambo mbalimbali yanayoendelea na yatakayotokea na vitatangaza maamuzi yake kwa wote.

“Kumekuwa na taarifa zikienea kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kwamba Mkurugenzi wa Mambo ya Nje CUF, Ismail Jussa amemnukuu Maalim Seif akisema kwamba Profesa Lipumba asahau uenyekiti CUF.

“Taarifa hii ni uongo na Katibu Mkuu hajaitoa. Hii ni miongoni  mwa propaganda zinazotengenezwa na watu wasio na malengo mema kwa chama, wakijua fika kwamba maamuzi ya chama hayafanywi na mtu bali vikao vya chama,” alisema Bimani katika taarifa hiyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles