30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

CRDB yawahamasisha wazazi, walezi kutumia Junior Jumbo

motherNa GUSTAPHU HAULE, PWANI

MENEJA wa Benki ya CRDB, tawi la  Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Nitike Nsekela, amewahamasisha wazazi wilayani hapa kutumia akaunti maalumu ya watoto iitwayo Junior Jumbo ili iweze kuwasaidia katika kuwaandalia maisha yao.

Nsekela alitoa wito huo juzi katika kilele cha maonyesho ya wajasiriamali yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mwanakalenga mjini Bagamoyo na kuwashirikisha wajasiriamali 280 kutoka mikoa mitano ya Kanda ya Mashariki.

Alisema CRDB ilianzisha akaunti ya Junior Jumbo kwa kutambua umuhimu wa watoto na kwamba utumiaji wake unasaidia kuhakikisha mtoto anapata maandalizi mazuri ikiwamo katika elimu.
Kwa mujibu wa Nsekela, akaunti hiyo inawahusu zaidi watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kwa kuwa kazi yake kubwa ni kuweka akiba kwa ajili ya watoto.

“Wazazi wengi wamekuwa wakipata shida hasa pale watoto wao wanapopata matatizo na hata wanapofikia umri wa kusoma. Kwa kulitambua hilo, CRDB iliamua kuja na mfumo wa akaunti hii kwa ajili ya kuwasaidia watoto nchini.

“Sifa kubwa ya akaunti hiyo ni kwamba inaweza kuendeshwa kwa kutumia shilingi ya Tanzania na hata fedha za kigeni kwa sababu lengo kuu ni kuwasaidia watoto.

“Pamoja na hayo, jambo la kuzingatia hapa ni kwamba, mtoto anapofikisha umri wa miaka 18, akaunti hubadilishwa na kuwa akaunti maalumu itakayokuwa ikitumika kwa malengo maalumu ya mhusika,” alisema Nsekela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles