22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

CHINA KUPIGA MARUFUKU MAGARI YANAYOTUMIA MAFUTA

SHANGHAI, CHINA

CHINA yenye soko kubwa zaidi la magari duniani, ina mpango ya kupiga marufuku uundaji na uuzaji wa magari yanayotumia dizeli na petrol.

Naibu Waziri wa Viwanda nchini humo, Xin Guobin, alisema jana kuwa umefanyika utafiti lakini bado hawajaamua ni lini amri hiyo itaanza kutekelezwa.

“Hatua hizo bila shaka zitaleta mabadiliko makubwa katika sekta yetu ya magari,” alisema Guobin.

China ilitengeneza magari milioni 28 mwaka uliopita  ikiwa ni takriban theluthi moja ya magari yote yaliyotengenezwa duniani.

Uingereza na Ufaransa tayari zimetangaza mipango ya kupiga marufuku magari mapya yanayotumia dizeli na petroli ifikapo mwaka 2040 kama sehemu ya hatua za kuzuia uchafuzi wa hali ya hewa duniani.

Kampuni ya China ya kutengeneza magari ya Volvo, ilisema Julai mwaka huu kuwa magari yake yatatumia umeme ifikapo mwaka 2019.

Makampuni mengine duniani yakiwamo Renault-Nissan, Ford na General Motors yote yanashughulikia mipango ya kutengeneza magari yanayotumia umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles