33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MIILI ILIYOHIFADHIWA KABURINI KARNE YA 16 YAGUNDULIWA MISRI

CAIRO, MISRI

MIILI ya mwanamke na watoto wake waliokuwa wamehifadhiwa karne kadhaa zilizopita  imegunduliwa na wana ekolojia jana, ikiwa katika kaburi linaloaminika kuwa la karne ya 16 hadi 11 BC.

Kaburi hilo lilipatikana karibu na Mji wa Luxor kilomita 70 kutoka   Cairo ambako kati ya vifaa vilivyopatikana ni sanamu ya mfua vyuma Amenemhat akiwa ameketi kando na mke wake.

Kwa mujibu wa wanasayansi  hao, mama alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 50 na uchunguzi ulionyesha kuwa alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa mifupa.

Watoto wawili wa kiume walikuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 30 na walikuwa wamehifadhiwa katika hali nzuri, kwa mujibu wa taarifa hizo jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles