22.1 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AUSTRALIA AUNGA MKONO USHOGA

SYDNEY, AUSTRALIA

WAZIRI Mkuu wa Australia, Malcolm Turnbull na viongozi kadhaa wa siasa nchi humo, wameunga mkono kampeni ya ndoa za jinsia moja.

Zaidi ya watu 20,000 walikusanyika mjini Sydney katika kampeni kabla ya kura ya maoni isiyo rasmi ya kubadilishwa sheria za ndoa nchini humo.

Turnbull alijitokeza ghafla na kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa katika Jimbo la New South Wales.

Baada ya hotuba hiyo, kiongozi wa upinzani nchini humo, Bill Shorten, alihutubia   mkutano mkuu wa chama chake naye akiunga mkono ndoa hizo.

Kura hiyo ya kubadilisha sheria ya ndoa inapigwa kwa njia ya posta kuanzia Septemba 12 na matokeo yakitarajiwa kutolewa Novemba mwaka huu.

Kura hiyo haitakuwa na uwezo wa kuhalalisha ndoa ya jinsia moja, lakini itachangia kupigwa kura bungeni kuona iwapo asilimia kubwa na watu Australia wataunga mkono mabadiliko hayo.

Awali, Waziri Mkuu huyo alisema binafsi atapiga kura kuunga mkono ndoa ya jinsia moja lakini hajafanya kampeni hadharani kabla ya hotuba yake ya jana.

Waziri Mkuu Turnbull alisema nchi nyingine 23 tayari zimehalalisha ndoa ya jinsia moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles