28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

KIMBUNGA IRMA CHAENDELEA KULETA UHARIBIFU FLORIDA

FLORIDA, MAREKANI

KIMBUNGA cha Irma kimevikumba  visiwa  Kusini mwa Jimbo la Florida,   Marekani kikiwa katika kiwango cha daraja la nne, kwa mujibu wa watabiri wa hali ya hewa.

Kimbuga hicho kilitarajiwa kuvikumba visiwa na upepo wa kasi ya hadi kilomita 209 kwa saa kabla ya kuelekea Kaskazini Magharibi kwa ghuba ya Florida.

Zaidi ya watu milioni 6.3 walitakiwa kuondoka Florida ambako kimbunga hicho kilitarajiwa   kuwa tishio kwa maisha ya wakazi wake.

Tayari kimbunga cha Irma kimeharibu baadhi ya visiwa  vya Caribbean, ikiwamo Cuba, ambako takribani watu 25 wamefariki dunia.

Viwango vya maji tayari vimeanza kuogezeka katika maeneo ya pwani ya Florida, eneo ambalo linatarajiwa kukumbwa na kimbunga kikubwa.

Wakati hali ikiwa hivyo  Florida, kumekuwa na taharuki juu ya hatma ya   Mji wa Tampa ambao uko kwenye njia ambayo kimbunga hicho kinatarajiwa kupitia.

Imeelezwa kuwa Tampa ni mji ulioko katika mazingira magumu zaidi nchini Marekani, hasa kuhusiana na hatari ya kukumbwa mara kwa mara na vimbunga.

Maofisa wa  Jimbo la Florida wametangaza hali ya tahadhari   katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo likiwamo jiji la Miami.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles